tokea masaa 19
Sudan imepokea shehena wa kwanza wa vifaa vya ujenzi wa umeme katika Jimbo la Khartoum, hii ikiwa ni ishara ya kuanza kwa juhudi za kurejesha umeme katika mji mkuu ambao miundombinu yake iliharibiwa kutokana na vita, ripoti za Shirika la Habari la Sudan (SUNA) zinasema.
Kampuni ya Umeme ya Sudan ilitangaza kuwasili kwa vinu 400 vya umeme vyenye uwezo tofauti, vilivyotengwa mahsusi kwa ajili ya kurekebisha mtandao wa gridi ya taifa mjini Khartoum.
ZILIZOPENDEKEZWA
Kwa mujibu wa Baraza la Uratibu wa Vyombo vya Habari la kampuni, uwasilishaji huo unaashiria uzinduzi mkubwa wa mpango wa ujenzi upya wa mji mkuu.


















