| Swahili
UTURUKI
3 dk kusoma
Uturuki kuanzisha uzalishaji wa wingi wa ndege ya mafunzo ya juu ya Hurjet: maafisa
Sampuli ya awali ya ndege hiyo imekamilisha zaidi ya saa 260 za safari za majaribio huku Uturuki ikijiandaa kusaini mkataba wa mauzo na Hispania.
Uturuki kuanzisha uzalishaji wa wingi wa ndege ya mafunzo ya juu ya Hurjet: maafisa
Uturuki kuanzisha uzalishaji wa wingi wa ndege ya Hurjet.
tokea masaa 13

Uturuki inaendelea kusonga mbele katika majaribio, maandalizi ya uzalishaji wa wingi na mipango ya kuuza ndege yake ya kwanza ya mafunzo ya juu iliyotengenezwa nchini, Hurjet, baada ya sampuli mbili ya awali ya ndege kukamilisha takribani safari 340 na saa 260, kulingana na maafisa wa ulinzi wa nchi hiyo.

Ndege hiyo, iliyotengenezwa na kiwanda cha anga cha Uturuki (Turkish Aerospace Industries), imepangwa kukabidhiwa kwa kikosi cha Jeshi la Anga la Uturuki, Turkish Stars, mwaka 2026. Kazi ya kuunganisha ndege zitakazokabidhiwa inaendelea, na ndege mpya inatarajiwa kufanya safari yake ya kwanza robo ya kwanza ya mwaka ujao.

Mradi wa Hurjet ulianza Agosti 2017, na ndege hiyo ilifanya safari yake ya kwanza Aprili 2023.

Kabla ya hapo, sehemu ya kwanza iliyokamilika iliingia katika hatua ya mwisho ya uunganishaji mwezi Juni 2022, ikifuatiwa na majaribio ya ardhini yaliyohusisha majaribio ya magurudumu ya kutua, ukaguzi wa mfumo wa nyaya, utendaji, pamoja na majaribio kamili ya mifumo ya avioniki, umeme na mafuta.

Ndege hii ya mafunzo yenye injini ya jeti na uwezo wa kasi ya juu iliwasha injini yake kwa mara ya kwanza tarehe 30 Januari 2023, kisha kufanya safari yake ya kwanza tarehe 25 Aprili 2023. Tangu wakati huo, majaribio yameendelea ndani ya viwango vya usanifu wake.

Wakati wa majaribio, ndege mbili za Hurjet zilifanya safari ya pamoja zikiwa na kamoflaji tofauti , na nyingine ikaruka pamoja na kikosi cha Turkish Stars, maonyesho yaliyovutia umakini mkubwa.

Kiwanda cha (TAI) inaanzisha mnyororo wa uzalishaji wenye uwezo wa kutengeneza ndege mbili kwa mwezi. Jeshi la Anga la Uturuki linatarajiwa kupokea ndege 16, na idadi hiyo itatarajiwa kuongezeka kadri matoleo mapya yatakavyozinduliwa.

Ndege hii yenye injini moja imetengenezwa kwa ajili ya mafunzo ya kisasa ya wapiganaji wa angani, doria zenye silaha na zisizo na silaha, pamoja na maonyesho ya vipeperushi (aerobatics).

Ina urefu wa mita 13.6, urefu wa mita 4.1 na upana wa mabawa wa mita 9.5. Inaweza kufikia kasi ya hadi Mach 1.4 na kuruka hadi futi 45,000. Hurjet ina maeneo saba ya kubebea mizigo mbalimbali, yenye uwezo wa kubeba hadi tani tatu.

Kiwanda hicho kinajiandaa kusaini mkataba wa kuiuza Hurjet kwa Hispania, huku mkataba wa mwisho ukitarajiwa kukamilika muda mfupi ujao, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa (TAI), Mehmet Demiroglu, alipozungumza na chombo cha habari cha Kihispania, El Espanol.

Demiroglu alisema kuwa ndege hiyo kimsingi ni ya mafunzo, lakini inaweza kubadilishwa kwa haraka kwa majukumu mengine au kutolewa katika matoleo tofauti kulingana na mahitaji ya mteja. Maelezo ya matoleo na ratiba kamili ya usambazaji yatabainishwa baada ya kutiwa saini kwa mkataba.

Mkataba huo unatarajiwa kujumuisha ununuzi wa takribani ndege 45 za Hurjet kwa ajili ya kuchukua nafasi ya ndege za kongwe za F-5 za Jeshi la Anga la Hispania, kwa thamani inayokadiriwa kufikia euro bilioni 3.12 (sawa na dola bilioni 3.6). Usafirishaji wa ndege hizo unatarajiwa kuanza mwaka 2028.

CHANZO:AA