UTURUKI
3 dk kusoma
Israel inaishutumu 'Uturuki chini ya utawala wa Erdogan’ kuwa na uhasama mkali dhidi yake
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel anasema Uturuki chini ya utawala wa Rais Erdogan "iliongoza sio tu kauli za uhasama bali pia hatua za kidiplomasia na kiuchumi dhidi ya Israel."
Israel inaishutumu 'Uturuki chini ya utawala wa Erdogan’ kuwa na uhasama mkali dhidi yake
Erdogan daima amekua akiangazia masaibu ya Wapalestina. / / AA
tokea masaa 7

Israel imesema kwamba Uturuki, chini ya uongozi wa Rais Recep Tayyip Erdogan, imeweka hatua za kidiplomasia na kiuchumi dhidi ya Tel Aviv kutokana na vita vya Israel dhidi ya Gaza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israeli, Gideon Saar, alisema Jumatatu kuwa msimamo wa Uturuki dhidi ya Israel umezidi kauli za maneno pekee.

“Uturuki, chini ya Erdogan, imeongoza uhasama dhidi ya Israel,” akibainisha “si tu kwa kauli za uhasama, bali pia hatua za kidiplomasia na kiuchumi,” Saar alisema kwenye mkutano wa pamoja na mwenzake wa Hungary, Peter Szijjarto, mjini Budapest, kama ilivyochapishwa na tovuti ya habari ya The Times of Israel.

Rais wa Uturuki Erdogan ameikosoa vikali Israel kwa mauaji ya halaiki yanayofanyika Gaza, ambapo zaidi ya watu 68,500 wamepoteza maisha tangu Oktoba 2023, na ametoa wito wa umoja wa Waislamu dhidi ya Israel.

Rais alisema mwezi Septemba kuwa wasiwasi wa Uturuki unazidi mipaka yake, akisisitiza mshikamano na mataifa ya Kiaislamu yanayopitia migogoro.

“Nusu ya moyo wetu ipo hapa; nusu nyingine ipo Gaza, Palestina, Yemen na Sudan, ambapo majeraha ya ulimwengu wa Kiislamu yanatiririka damu,” Erdogan amesema.

Mnamo Mei 2, 2024, Uturuki ilisitisha kabisa operesheni zote za mauzo ya nje, kuingiza bidhaa, usafirishaji wa bidhaa zote na Israel, ikikomesha shughuli zote za kibiashara, ikiwemo mchakato wa forodha na biashara za maeneo ya huru kati ya nchi hizi mbili.

Majibu makali dhidi ya Israel

Mnamo Septemba, Erdogan alimkosoa vikali Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwa shambulio la Israel dhidi ya wasuluhishi wa Hamas nchini Qatar, akisema: “Kifikra, Netanyahu ana uhusiano na Hitler.”

“Kama Hitler hakuweza kuona mwisho wa kushindwa kwake, Netanyahu atakabiliana na hatima ile ile,” alisema.

Erdogan pia alisema kuwa mipango ya “kufanya eneo letu liwe na utulivu wa kutokuwa na uhakika” haitafanikiwa na “mabeberu na Kizayuni wenye kuendesha umwagaji wa damu” hawawezi kufanikisha malengo yao.

“Majibu makali zaidi kwa mauaji haya ya miezi 23 ambayo hayakuwahi kuonekana yametoka tena kutoka Uturuki na wananchi wake,” Erdogan alisema.

Erdogan pia alitoa hotuba kali katika mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York mwezi Septemba, akiishutumu Israel kutekeleza mauaji ya halaiki Gaza na akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua haraka kumaliza damu inayomwagika.

Trump anampongeza Erdogan

Vita vya Israel vilisimama baada ya mkataba wa kusitisha mapigano kuanza Oktoba 10, chini ya mpango wa pointi 20 wa Rais wa Marekani, Donald Trump.

Trump alimshukuru mwenzake wa Uturuki, Erdogan, kwa msaada wake katika kuunda mkataba wa kusitisha mapigano Gaza.

“Bwana huyu kutoka nchi inayoitwa Uturuki ana jeshi moja la nguvu zaidi duniani, kweli kabisa. Ni lenye nguvu zaidi kuliko anavyotaka wengine wajue,” Trump alisema wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa kusitisha mapigano Gaza Sharm el-Sheikh.

Uturuki iliendelea kuthibitisha kusimamishwa kwa biashara zote na Israel mnamo Agosti, huku Waziri wa Mambo ya Nje akitangaza kwamba meli za Kituruki hazitaruhusiwa tena kufika kwenye bandari za Israel na ndege za Israel hazitaruhusiwa kutumia anga la Uturuki.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, pia alisema kuwa ukaidi wa Wapalestina dhidi ya Israel “utabadilisha mwelekeo wa historia, utakuwa ishara kwa waliokandamizwa, na utajenga misingi ya mfumo uliyofeli.”

 

 

 

 

CHANZO:TRT World