Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesisitiza kuhusu jitihada za nchi yake kusema ukweli kwa yanayofanyika Gaza na kuhakikisha kuwa "haki inapatikana."
"Uturuki itaendelea kupambana kwa kila njia kuhakikisha kuwa yanayofanyika Gaza hayasahauliki na kwamba haki inapatikana,” Erdogan alisema siku ya Alhamisi katika hotuba kwenye hafla ya tuzo za utamaduni na sanaa mji mkuu wa Ankara.
"Kama nchi na serikali tumedhamiria kusema ukweli," aliongeza, Uturuki inasimama kikamilifu na watu wa Palestina, "hatuteteleki na bila wasiwasi.”
Vyombo vya habari ‘jasiri’
Erdogan pia alipongeza vyombo vya habari vya Uturuki kwa misimamo ya "kijasiri" katika kuangazia ukweli ya yale yanayofanyika Gaza.
"Huku mauaji ya halaiki yakitokea Gaza, vyombo vya habari vya Uturuki, hasa TRT na Anadolu, vimechukuwa hatua za kijasiri," kiongozi huyo wa Uturuki alisema.
Akimpongeza mpiga picha wa Anadolu Ali Jadallah, Erdogan alisema: “Kinachoonekana kupitia upigaji picha wake siyo tu kinaonesha ukatili wa mauaji Gaza lakini pia upambanaji wa haki wa watu wa Palestina ili dunia ipate kuona.”
“Kaka yetu Ali, ambaye ameonesha mauaji ya kikatili ya halaiki Gaza na kuonesha kile ulimwengu unaosemekana kuwa wa kistaarabu ukweli, anafanya kazi kama mpiga picha wa Anadolu," alisema.






















