| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Droni zimewaua raia zaidi ya 100 Sudan tangu Disemba 4: Umoja wa Mataifa
Watu wasiopungua 104 wameuawa, ikiwemo watoto 43, katika mashambulizi mbalimbali eneo la Kordofan nchini Sudan tangu Disemba 4, ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu ilisema siku ya Jumanne.
Droni zimewaua raia zaidi ya 100 Sudan tangu Disemba 4: Umoja wa Mataifa
Mwanajeshi akizima moto kufuatia mashambulizi ya droni mji wa Ad-Damar mashariki mwa Sudan. / Reuters
tokea masaa 8

Watu wasiopungua 104 wameuawa, ikiwemo watoto 43, katika mashambulizi mbalimbali eneo la Kordofan nchini Sudan tangu Disemba 4, ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu ilisema siku ya Jumanne.

"Nimeshtushwa na kuongezeka kwa mashambulizi," amesema Mkuu wa Masuala ya Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk, akieleza kuhusu mapigano kati ya Jeshi la Sudan, vikosi vya Rapid Support Forces na Sudan People's Liberation Movement-Kaskazini huko Kordofan, eneo ambalo lina majimbo matatu katikati na kusini mwa Sudan.

Hakutoa maelezo mahsusi zaidi kuhusu nani anayehusika na mashambulizi hayo ya ndege zisizo na rubani, ambayo anasema ilishambulia hospitali, shule ya chekechea na kambi ya Umoja wa Mataifa.

Serikali ya Sudan imekuwa ikishtumu wapiganaji wa RSF kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani kuwalenga raia, madai ambayo kundi hilo inakanusha.

CHANZO:AA