| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Mkuu wa majeshi Sudan Burhan yuko tayari kwa mazungumzo kuhusu amani na Trump
Jenerali Abdel Fattah al Burhan amepongeza "dhamira ya mazungumzo na juhudi za kutafuta na kumaliza vita nchini kwake" za Trump.
Mkuu wa majeshi Sudan Burhan yuko tayari kwa mazungumzo kuhusu amani na Trump
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan akitembelea kambi ya Al-Afadh huko Al Dabbah, Jimbo la Kaskazini. / AA
tokea masaa 10

Mwenyekiti Baraza la Mpito la Sudan Abdel Fattah al-Burhan yuko tayari kufanya kazi na Rais wa Marekani Donald Trump kwa lengo la kumaliza mgogoro unaogawanya nchi, wizara ya mambo ya nje imesema siku ya Jumanne.

Wizara hiyo ilitoa taarifa hiyo baada mkuu huyo wa majeshi kufanya ziara mjini Riyadh kama mgeni wa Mwanamfalme Mohammed bin Salman, ambaye hivi majuzi aliwasilisha mapendekezo ya amani Sudan kwa Trump katika ziara ya hivi karibuni jijini Washington.

Kulingana na taarifa ya Sudan, Burhan alipongeza "dhamira ya mazungumzo na juhudi za kutafuta na kumaliza vita nchini kwake" za Trump, na kwa ushiriki wa Saudi Arabia.

"Alithibitisha utayari wa Sudan kufanya kazi na Rais Trump, waziri wake wa mambo ya nje, na mjumbe wake kuhusu amani ya Sudan kwa kutimiza lengo hili la msingi," ilisema, akizungumzia kuhusu Marco Rubio na Mjumbe wa Marekani Massad Boulos.

Changamoto za kidiplomasia

Juhudi za amani za kimataifa zilizoongozwa na wapatanishi kutoka Marekani, Misri, Saudi Arabia na Imarati zimekwama tangu Burhan alipokataa mapendekezo ya mwisho ya Boulos.

Jenerali huyo alishtumu wapatanishi kwa kuegemea upande mmoja na kuzungumzia maelekezo ya UAE, ambayo wanaishtumu kwa kuwapa na kuwaunga mkono wapinzani wao wapiganaji wa RSF.

UAE imekuwa ikikanusha kuwa inapeleka silaha, mafuta na wapiganaji kwa RSF, licha ya uchunguzi huru na ripoti za kimataifa kudai tofauti.

CHANZO:TRT Afrika