| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
AFCON inastahili heshima kama ilivyo kwa Kombe la Dunia, anasema nyota wa Nigeria Chukwueze
Wanaiweka katika ratiba (AFCON) wakati mbaya, lakini kusema kuwa siyo mashindano yanayostahili au makubwa haikubaliki, anasema mshambuliaji wa Nigeria Samuel Chukwueze.
AFCON inastahili heshima kama ilivyo kwa Kombe la Dunia, anasema nyota wa Nigeria Chukwueze
Mashabiki wa soka wa Nigeria wakiwa na mfano wa kombe la AFCON. / Reuters
25 Desemba 2025

Mshambuliaji wa Nigeria Samuel Chukwueze anaamini kuwa mashindano ya Kombea la Mataifa ya Afrika yanatakiwa kupewa heshima sawa na hadhi ya Kombe la Dunia na Ligi ya Mabingwa ya Ulaya kufuatia utata kuhusu muda wa michezo hiyo nchini Morocco.

Kwanza ilipangiwa kufanyika miezi ya Juni na Julai, sasa AFCON ya mwaka huu inachezawa Disemba 21-Januari 18, kuwapokonya vilabu vya Ulaya wachezaji wao muhimu wanaocheza kwenye timu za taifa kipindi ambacho ni muhimu kwa ligi za maeneo hayo.

"Kila mtu anataka kucheza AFCON. Ni moja ya mashindano muhimu duniani," Chukwueze ameiambia On Sports TV.

"Lazima uheshimu AFCON sawa sawa kama unavyoheshimu mashindano ya Ulaya au Kombe la Dunia."

"Tunaelewa wameratibu mechi hizi katika kipindi kibaya cha mwaka, lakini inapokuwa muhimu, ukihitajika unaitwa na unakwenda," alisema.

"Hauna hiari, klabu yako haiwezi kukuzuia na hakuna mtu anayeruhusiwa kusema chochote kibaya kuhusu AFCON. Ndiyo, wanaiweka wakati mbaya, lakini kusema siyo mashindano mazuri au makubwa si sahihi."

Chukwueze aliisaidia Nigeria kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Tanzania katika mechi yao ya ufunguzi ya kundi C huku wakisubiri mechi yao ya pili dhidi ya Tunisia siku ya Jumamosi.

CHANZO:TRT Afrika Swahili