AFRIKA
2 dk kusoma
Jopo la mawakili wa makamu wa Rais wa Sudan Kusini wasema wako tayari kwenda mahakamani
Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar ameshtakiwa kwa mauaji, uhaini na uhalifu dhidi ya binadamu.
Jopo la mawakili wa makamu wa Rais wa Sudan Kusini wasema wako tayari kwenda mahakamani
Makamu wa Rais wa Sudan Kusini amekuwa kizuizini tangu Machi 2025/ picha: Reuters
tokea masaa 2

Timu ya utetezi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Sudan_Kusini, Riek Machar, na washtakiwa wengine saba imesema iko tayari kwa kesi itakayowakilishwa.

“Septemba 12, sisi kama timu ya wanasheria ya Riek K Machar tulimtembelea alipo kizuizini. Hii ilikuwa mara ya kwanza yeye kutembelewa tangu 26 machi 2025 alipokamatwa na kuwekwa kizuizini nyumbani,” timu hiyo ilisema katika taarifa iliyoandikwa na Kur and Co Advocates, kwa niaba ya timu yake ya mawakili.

“Tunaangalia hii kama msingi muafaka wa kuhakikisha haki katika kesi na kulinda haki za mtuhumiwa kuwasiliana na baraza lake la sheria,” taarifa iliongezea.

Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar ameshtakiwa kwa mauaji, uhaini na uhalifu dhidi ya binadamu.

Waziri wa Sheria nchini humo alisema kuwa Machar alihusika katika mashambulizi ya wanamgambo wa kikabila dhidi ya vikosi vya serikali mwezi Machi.

Machar amekuwa katika kizuizi cha nyumbani tangu mwezi Machi kuhusiana na mashambulizi ya wanamgambo maarufu" white army" ambao walishambulia mji wa kaskazini mashariki wa Nasir, mwezi Machi.

Mashambulizi hayo yalisababisha kifo cha meja jenerali wa jeshi la Sudan Kusini na zaidi ya wanajeshi wengine 250 pamoja na wanawake na marubani wa Umoja wa Mataifa.

Saa chache baada ya tangazo la kumpata Machar na kesi ya kujibu, Rais Salva Kiir alimsimamisha Machar kutoka wadhifa wake, kupitia amri iliyosomwa kwenye redio ya serikali.

Kando na Machar, watu wengine 20 walifunguliwa mashtaka katika kesi hiyo. Kumi na tatu kati ya hao hawajakamatwa.

Timu ya mawakili imesema iliweza kuwatembelea washitakiwa wengine wanne katika maeneo yao wanayozuiliwa na bado haijapata nafasi ya kuwatembelea wengine watatu.

“Kesi hii kwa asili yake na kutokana na utata wake wa kisiasa na kisheria inahitaji kuongozwa na misingi ya haki na ukweli,” mawakili wa Machar wamesema.


CHANZO:TRT Swahili