Uturuki imekemea vikali uhalifu unaofanywa na Kikosi cha RSF, nchini Sudan, dhidi ya raia.
"Tunakemea vikali uhalifu unaofanywa na RSF dhidi ya raia na tunaitisha upatikanaji wa haraka wa misaada ya kibinadamu katika mikoa husika," mjumbe wa Uturuki kwenye Umoja wa Mataifa Ahmet Yildiz aliwaambia wajumbe wa Baraza la Usalama la UN kuhusu Sudan Jumatatu.
Yildiz alisema Sudan imekuwa "mgogoro mkubwa kabisa wa watu waliohama makazi" duniani na kwamba Ankara imehuzunika kutokana na yaliyojiri hivi karibuni huko Al Fasher na mkoa wa Kordofan.
Alikemea pia shambulio la RSF la Disemba 13 dhidi ya kambi ya vifaa ya Jeshi la Mpito la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Abyei huko Kadugli, Kordofan Kusini, ambalo liliuwa walinda amani sita wa Bangladeshi na kujeruhi wengine nane.
"Uturuki inaelezea umoja wa Sudan, utegemezi wa mipaka yake, uhuru wake kama moja wapo ya misingi ya sera zetu za kanuni kwa eneo na Afrika kwa ujumla," aliongeza.
"Ni kwa njia ya halali na mazungumzo pekee ndipo suluhisho endelevu la mgogoro linaweza kupatikana," Yildiz alisema, akiunga mkono juhudi za kikanda na za kimataifa za kusimamisha vita.
"Juhudi za jamii ya kimataifa zinapaswa kugeuzwa kuwa mchakato wa amani jumuishi ambao utawezesha kusitishwa kwa mapigano kwa muda mrefu ukifuatiwa na mchakato mpana wa kisiasa na uwajibikaji," aliongeza.
Uturuki inaendelea kujihusisha na Sudan
Akitaja kujihusisha kwa Uturuki na Sudan, alisema meli za misaada za Uturuki zimetuma karibu tani 10,000 za msaada, wakati vifaa vya matibabu vimetumwa kupambana na kipindupindu, na mahema 30,000 yako njiani kuelekea Sudan.
"Watu wa Sudan wanapaswa kuondolewa katika mtego wa vurugu na kifo," Yildiz aliongeza.
RSF imekuwa katika vita na jeshi la Sudan tangu Aprili 2023.
Mnamo Oktoba 26 mwaka huu, majeshi ya RSF yaliingilia Al Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, baada ya kuzingirwa kwa siku 500, na kusababisha mauaji ya kimbari, uhamisho mkubwa wa watu, na kuacha raia waliokwama wakiwa na upungufu mkubwa wa chakula.





















