Katibu Mkuu wa UN aeleza wasiwasi wake kuhusu Tanzania
Machafuko yalizuka katika sehemu tofauti nchini humo tangu 29 Oktoba 2025 huku waandamanaji wakipinga uchaguzi huo na kutaka mabadiliko.
Katibu Mkuu wa UN aeleza wasiwasi wake kuhusu Tanzania
Katibu Mkuu wa UN ameonyesha wasiwasi kuhusu hali nchini Tanzania / Reuters
tokea masaa 8

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , Antonio Guterres ameeleza wasiwasi wake kuhusu hali ilivyo nchini Tanzania.

Machafuko yalizuka katika sehemu tofauti nchini tangu 29 Oktoba 2025 huku waandamanaji wakipinga uchaguzi huo na kutaka mabadiliko.

“ Ikiwa ni pamoja na ripoti za vifo na majeruhi wakati wa maandamano. Ninatoa wito kwa wote kujizuia, kukataa vurugu na kushiriki katika mazungumzo ya pamoja na yenye tija ili kuzuia kuongezeka kwa vurugu, “ Guterresalisema katika ujumbe kwa mtadao wa X.

Katibu Mkuu ametaka “uchunguzi wa kina na usiopendelea upande wowote kuhusu tuhuma zote za matumizi ya nguvu kupita kiasi,” na kuzitaka mamlaka za Tanzania kuzingatia uwajibikaji na uwazi katika kushughulikia machafuko ya baada ya uchaguzi.

“Umoja wa Mataifa (UN), uko tayari kuunga mkono juhudi zinazolenga kuleta majadiliano, kuimarisha utawala wa kidemokrasia na kuendeleza amani endelevu nchini Tanzania,” aliongeza.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR, pia iliripoti kuwa amri ya kutotoka nje nchini kote kuanzia saa kumi na mbili jioni inaendelea huku huduma za intaneti zikionekana kuwa na vikwazo vingi tangu siku ya kupiga kura.

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ilizitaka mamlaka kurejesha huduma ya mtandao mara moja na kuwezesha wananchi kufikia kwa ukamilifu haki zao za msingi ikiwemo uhuru wa kujieleza, kujumuika na kukusanyika kwa amani.

Waandamanaji pia walitakiwa kuandamana kwa amani.