Rais wa Gambia Adama Barrow
Rais wa Gambia Adama Barrow
Rais wa Taifa la Gambia au The Gambia ni Adama Barrow mwenye umri wa miaka 60.
22 Oktoba 2025

 Adama Barrow ndiye aliyemtoa madarakani kwa njia ya uchaguzi kiongozi aliyekuwepo kwa zaidi ya miaka ishirini, Yahya Jammeh.

Alizaliwa eneo la Mankamang Kunda,katika wilaya ya Jimara,Mashariki mwa Gambia.Mwanzoni mwa miaka ya 2000 alielekea London, Uingereza huko alifanya kazi pamoja na biashara na mwaka 2006 akarudi Gambia alipoendeleza biashara zake.

Alikuwa mweka hazina wa chama cha upinzani UDP na baadaye kuwa kiongozi baada ya aliyekuwa kinara wake kufungwa jela 2016.

Katika uchaguzi wa urais wa 2016 alikuwa mgombea wa upinzani akiwakilisha muungano wa vyama mbalimbali.

Alishinda uchaguzi huo kwa kupata kura asilimia 43.34 na kumshinda kiongozi wa muda mrefu Yahya Jammeh.

Jammeh kwanza alikubali matokeo hayo, lakini baadaye akabadilisha msimamo, jambo lililofanya akimbie katika nchi jirani ya Senegal.

Aliapishwa akiwa katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal Januari 2017, ikawa zamu ya Jammeh kukimbia nchini na Barrow akarudi kuapishwa rasmi.

Rais huyu Adama Barrow ambaye wakati mwingine huonekana akiwa na wake zake wawili aligombea tena uchaguzi wa 2021 na akapewa mitano tena.

Kutokana na kuwa katiba mpya ambayo ina ukomo wa mihula haijapitishwa, na tayari ameshathibitisha kuwa atagombea muhula wa tatu 2026, katika nchi hiyo ya Gambia moja ya taifa dogo zaidi barani Afrika.  

 

CHANZO:TRT Afrika Swahili