| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Waliowasababishia mateso watu wa Gaza ‘watawajibishwa’: Erdogan
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema atafanya mazungumzo ya simu na Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatatu kujadili hali ya Gaza pamoja na juhudi za amani kati ya Ukraine na Urusi.
Waliowasababishia mateso watu wa Gaza ‘watawajibishwa’: Erdogan
Erdogan na Trump kuzungumza kwa njia ya simu siku ya Jumatatu, Rais wa Uturuki alisema. / / AA
tokea masaa 12

Rais Erdogan ameyapongeza maandamano makubwa ya kuunga mkono Palestina yaliyofanyika Istanbul, Uturuki, siku ya Mwaka Mpya, akiyaita kuwa ya “kihistoria,” na kusema kuwa maandamano hayo yametuma ujumbe wazi kwamba “Palestina haiko peke yake.”

“Yale alioyafanya huyu Farao anayeitwa Benjamin Netanyahu (Waziri Mkuu wa Israel) hayatapita bila adhabu, kwa sababu amejiletea laana za watu wengi waliodhulumiwa, kuanzia watoto hadi wazee,” alisema Erdogan siku ya Ijumaa.

Akilaani vitendo vya Israel huko Gaza na hali mbaya ya kibinadamu inayozidi kuzorota, Rais huyo alisema: “Maumivu ya watoto wa Gaza, wanaoishi kwenye mahema ya muda huku wakikabiliwa na upepo na mvua, hayatopita bila ya uwajibikaji, na Netanyahu hataepuka kuwajibishwa.”

Rais wa Uturuki pia alisema kuwa yeye na Rais wa Marekani Donald Trump wanatarajiwa kuzungumza kwa simu siku ya Jumatatu, alisema hili baada ya swala ya Ijumaa.

“Tutaendelea na mazungumzo mengine na Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatatu,” Erdogan alisema mjini Istanbul, akiongeza kuwa mazungumzo hayo yatafanyika mchana.

‘Hatutasahau Palestina’

Takriban watu 520,000 walikusanyika mapema siku ya Alhamisi, siku ya Mwaka Mpya, katika Daraja la Galata mjini Istanbul kwa maandamano makubwa ya kuunga mkono Palestina. Maandamano hayo yaliandaliwa chini ya muungano wa ‘Humanity Alliance na National Will Platform’.

Zaidi ya mashirika 400 kiraia walishiriki maandamano hayo, ambayo yameongozwa na Shirika la Vijana la Uturuki (TUGVA), yalifanyika chini ya kaulimbiu: “Hatutaogopa, hatutanyamaza, hatutasahau Palestina.”

Waliyoshiriki walitoa wito wa kusitishwa kwa mauaji ya halaiki huko Gaza.

Katika vita vya Israel dhidi ya Gaza vilivyoanza Oktoba 2023, zaidi ya Wapalestina 71,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, waliuawa na eneo hilo kuharibiwa vibaya. Ingawa makubaliano ya kusitisha mapigano yalianza kutekelezwa Oktoba 2025, ukiukaji kutoka upande wa Israel unaendelea.

CHANZO:AA