Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, siku ya Jumanne alimpokea Balozi wa Marekani nchini Uturuki, Tom Barrack, ambaye pia ni mjumbe maalum wa Syria.
Picha ya mkutano huo iliwekwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki kupitia mtandao wa kijamii wa X, bila ya kutoa maelezo zaidi.
Barrack alinukuu chapisho hilo hilo na kusema: “Kuendelea na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan leo.
Marekani ilikuwa imepongeza makubaliano mapya ya kusitisha mapigano na ya ujumuishaji kati ya serikali ya Syria na YPG siku ya Jumapili. “Makubaliano haya na usitishaji wa mapigano yanawakilisha hatua muhimu ya mabadiliko,” Barrack alisema kwenye X.
Alisema Rais wa Syria, Ahmed al Sharaa, amemthibitishia kuwa Wakurdi ni sehemu muhimu ya Syria, akiongeza: “Marekani inatazamia mchakato wa ujuimishaji utimie kwa mshirika wetu wa kihistoria katika mapambano dhidi ya Daesh.”
“Hatua ngumu ya kukamilisha maelezo ya makubaliano ya kina ya muungano inaanza sasa, na Marekani inasimama imara kuunga mkono mchakato huu katika kila hatua,” alisema.
Al Sharaa alitangaza siku ya Jumapili usitishaji kamili wa mapigano na makubaliano ya ujumuishaji kikamilifu kati ya serikali ya Syria na YPG, akieleza hatua pana za kurejesha mamlaka ya dola katika eneo la kaskazini-mashariki mwa nchi.
Kwa mujibu wa masharti yaliyochapishwa na Shirika la Habari la SANA, makubaliano hayo yanatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano katika nyanja zote na maeneo yote ya mawasiliano kati ya majeshi ya serikali na YPG.
Makubaliano hayo yanatarajiwa kuanza kutekelezwa sambamba na kuondolewa kwa vikosi vyote vya kijeshi vinavyohusishwa na YPG kuelekea maeneo ya mashariki mwa Mto Furat, kama hatua ya maandalizi kwa ajili ya kupanga upya vikosi.





















