| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan akosoa kuangaziwa duni kwa ukatili wa Israel dhidi ya wanawake huko Gaza
Rais wa Uturuki amesema bila kujali asili ya mnyanyasaji au anayenyanyaswa , Uturuki itasema ukweli kwa sauti kubwa katika kila jukwaa.
Erdogan akosoa kuangaziwa duni kwa ukatili wa Israel dhidi ya wanawake huko Gaza
Ukatili dhidi ya wanawake huko Gaza haujapokea mwitikio unaostahili, anasema rais wa Uturuki.
tokea masaa 12

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema kuwa ukatili unaofanywa dhidi ya wanawake huko Gaza haujapokelewa na kuangaziwa kwa njia inayostahili.

“Asili ya mtenda kosa na ya muathiriwa ndiyo tena imeamua namna dunia inavyoangazia,” Erdogan alisema katika hafla iliyofanyika mji mkuu Ankara, kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake, iliyoadhimishwa Jumanne.

Erdogan alitaja mauaji ya halaiki yanayofanywa na Israel dhidi ya Gaza, akieleza uzito wa uhalifu wa Israel dhidi ya Wapalestina.

“Theluthi mbili ya tatu ya Wapalestina 70,000 waliouawa katika mauaji ya halaiki Gaza ni, kwa bahati mbaya, wanawake na watoto. Hii ni takwimu ya kutisha kwa yeyote mwenye dhamiri.”

Akiita ukatili dhidi ya wanawake ukiukwaji wa msingi wa utu wa mwanadamu, Erdogan aliuainisha kama uhalifu wa kimataifa.

“Tutatetea yaliyo ya haki bila kujali asili ya mnyanyasaji au anayenyanyaswa, na tutasema ukweli kwa sauti kubwa katika kila jukwaa,” aliongeza.

“Kama rais na baba wa mabinti wawili, nitaendelea kuwa mstari wa mbele katika kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kama nilivyokuwa daima,” alisema katika hotuba yake kuu.

“Ukatili dhidi ya watu, hasa wanawake na watoto, ni uhalifu dhidi ya ubinadamu, ni usaliti kwa ubinadamu. Mkono na dhamiri ya yeyote anayenyanyua mkono wake dhidi ya mwanamke huchafuka,” alisema.

CHANZO:AA