| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Korea Kusini yawataka raia wake kuondoka Mashariki ya Kati
Ushauri huo unakuja wakati Israel ikiendelea kuishambulia Lebanon katika vita vya Marekani-Israel dhidi ya Iran
Korea Kusini yawataka raia wake kuondoka Mashariki ya Kati
Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo, imewataka raia wa nchi hiyo waiishio Lebanon, kuondoka mara moja Mashariki ya Kati./Picha:Wengine
tokea masaa 2

Korea Kusini imewataka raia wake kuondoka Lebanon huku kukiwa na ongezeko la mashambulizi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo, imewataka raia wa nchi hiyo waiishio Lebanon, kuondoka mara moja Mashariki ya Kati, kwa kutumia ndege zitakazopatikana.

Inakadariwa kuwepo na raia 120 wa Korea Kusini waishio Lebanon, kulingana na shirika la habari la Yonhap.

Mapema Jumatano, Korea Kusini iliweka zuio la safari za Lebanon.

Mashambulizi ya pamoja ya Marekani-Israel dhidi ya Iran, yalianza Februari 28, na kupelekea kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.

 

CHANZO:AA