| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Ivory Coast yamrejesha kikosini Wilfred Zaha kwa ajili ya fainali za AFCON
Zaha, mwenye umri wa miaka 33, ambaye kwa sasa anachezea timu ya Charlotte, inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Marekani, alikuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 26 ambacho kitakabaliana Msumbiji, Cameroon na Gabon kwenye Kundi F.
Ivory Coast yamrejesha kikosini Wilfred Zaha kwa ajili ya fainali za AFCON
Zaha aliondolewa kwenye kikosi cha Tembo hao mwaka jana./Picha:@CharlotteFC
tokea siku moja

Mabingwa watetezi wa Kombe la AFCON, Ivory Coast imemrudisha kikosini winga wa zamani wa Crystal Palace, Wilfried Zaha kwa ajili ya michuano ya AFCON 2025 itakayofanyika nchini Morocco.

Zaha, mwenye umri wa miaka 33, ambaye kwa sasa anachezea timu ya Charlotte, inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Marekani, alikuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 26 ambacho kitakabaliana Msumbiji, Cameroon na Gabon kwenye Kundi F.

Zaha aliondolewa kwenye kikosi cha Tembo hao mwaka jana, baada ya timu ya taifa ya Ivory Coast ilipopenya kwenye hatua ya mtoano, kabla haijafunga Nigeria kwa mabao 2-1 kwenye fainali iliyofanyika jijini Abidjan.

"Tunahitaji wachezaji wazoefu. Zaha ana uwezo wa kuwakabili mabeki," alisema kocha Emerse Fae wakati akitangaza kikosi hicho kwenye televisheni ya nchi hiyo.

Zaha, ambaye alishiriki michezo minne tu akiwa na Manchester United akiwa Old Trafford kwa misimu miwili kabla ya kurejea Palace, alishiriki michezo miwili ya kimataifa akiwa na jezi ya England, kabla ya kuhamia kuichezea Ivory Coast.

CHANZO:AFP