AFRIKA
1 dk kusoma
Shirika la ndege la Tanzania lazindua safari kati ya Dar es Salaam na Lagos
Uzinduzi wa kituo hicho, kilichopewa Mchongo namba 29, ulianza Septemba 19 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, na kuendelea Lagos siku iliyofuata.
Shirika la ndege la Tanzania lazindua safari kati ya Dar es Salaam na Lagos
Moja ya ndege za shirika la ATCL./Picha:Wengine
tokea masaa 9

Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) limezindua rasmi safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam na Lagos nchini Nigeria, hatua inayounganisha Afrika Mashariki na Magharibi kupitia sekta ya anga.

Kulingana na Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Peter Ulanga, safari hizo zinalenga kufungua fursa mpya za kibiashara, usafirishaji na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.

“Safari hizi zitafungua fursa mpya za kibiashara, usafirishaji na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia,” alisema Ulanga wakati wa uzinduzi wa safari hiyo.

Uzinduzi wa kituo hicho, kilichopewa Mchongo namba 29, ulianza Septemba 19 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, na kuendelea Lagos siku iliyofuata.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Selestine Kakele, kuanzishwa kwa safari hizo kutachochea biashara kati ya nchi hizo mbili.

“Nigeria ni mnunuzi mkubwa wa mkonge kutoka Tanzania, ikuchukua takribani asilimia 26 ya uzalishaji wote baada ya China. Bidhaa nyingine tunazosafirisha ni pamoja na ngozi, ambayo hapa hutumika kama chakula na malighafi viwandani. Safari hizi zitakuza biashara hizo,” alisema Balozi huyo.

CHANZO:TRT Afrika Swahili