Wako wapi wachezaji wa Kiafrika waliong'aa enzi zao katika ligi ya NBA ya mpira wa kikapu?
Mchezaji wa Mpira wa kikapu wa timu ya Minnesota Timberwolves, Luol Deng / Reuters
Wako wapi wachezaji wa Kiafrika waliong'aa enzi zao katika ligi ya NBA ya mpira wa kikapu?
Tuangalie baadhi ya wachezaji wa Kiafrika ambao walikuwa kwenye ligi ya NBA, tupate kufahamu wako wapi sasa hivi.

Kama ilivyo katika michezo mbali mbali huwa kuna ukomo au pengine kustaafu kwa mchezaji. Katika mchezo wa mpira wa kikapu pia wachezaji hufikia kipindi wakaamua kuondoka mchezoni.

Sababu zinaweza kuwa nyingi, kwa wengine ni umri kuwa mkubwa kushindwa kuhimili tena mikiki mikiki kama enzi za ujana, wengine ni majeraha, au wengine ni maamuzi tu.

Hebu tuangalie baadhi ya wachezaji ambao walikuwa kwenye ligi ya NBA, tupate kufahamu wako wapi sasa hivi.

LUOL DENG

Luol Ajou Deng alizaliwa Sudan miaka 39 iliyopita, na ana uraia pacha wa Sudan Kusini na Uingereza. Alianza kucheza katika ligi ya NBA mwaka 2004 akiwa na timu ya Phoenix Suns.

Alicheza pia katika timu za Chicago Bulls, Miami Heat, Los Angeles Lakers na Minnesots Timberwolves. Deng mwenye urefu wa futi 6 na inchi 9 alistaafu na kuanzia 2019 amekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Sudan Kusini.

Pia hujishughulisha na masuala ya kuwasaida wakimbizi.

HASHEEM THABEET

Ni raia wa Tanzania mwenye urefu wa futi 7 na inchi 3. Alianza kucheza mpira wa kikapu akiwa na umri wa miaka 15. Mwaka 2009 alikuwa mchezaji wa kwanza aliyezaliwa Tanzania kucheza katika ligi ya NBA, kipindi hicho akijiunga na timu ya Memphis Grizzlies.

Alicheza pia katika timu za Houston Rockets, Portland Trail Blazers na Oklahoma City Thunder. Thabeet mwenye umri wa miaka 37 pia alicheza katika ligi ya nje ya Marekani

na kufikia mwaka 2024 alikuwa amejiunga na timu ya nyumbani Tanzania Dar City na aliisaidia timu hiyo kupata mafanikio waliposhiriki mashindano ya kwanza ya mpira wa kikapu kwa timu za Afrika Mashariki.

DJ MBENGA

Didier ‘’D.J’’ Ilunga-Mbenga alizaliwa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 1980. Ana uraia pacha wa DRC na Ubelgiji.

Uhodari wake wa kucheza mpira wa kikapu ulionekana wakati alipokuwa anaishi Ubelgiji. Alipata fursa ya kucheza kwenye ligi kuu ya nchini humo akiwa na timu tofauti.

Alianza kucheza kwenye ligi ya NBA mwaka 2004. Mbenga mwenye urefu wa futi 7 kamili alikuwa katika timu za Dallas Mavericks, Golden State Warriors, Los Angeles Lakers na New Orleans Hornets.

Pia aliwahi kucheza katika ligi ya Ufilipino. Mwaka 2005 alianzisha wakfu wa Mbenga kwa lengo la kuwasaidia watoto nchini DRC pamoja na kuwapa usaidizi wakimbizi nchini Ubelgiji.

Safari ni hatua, wamevuma wakiwa kwenye ligi kubwa ya mpira wa kikapu duniani na wanaendelea kuvuma katika safari zao nyingine za maisha.


CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
Lamine Yamal: Mfalme aliyekosa taji la Ballon d'Or
Ukraine yapinga uamuzi wa kuipa Moscow uwenyeji wa Mashindano ya kunyanyua vyuma 2030
Kenya yafuzu hatua ya 16 bora katika Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake la U-17 kwa mara ya kwanza
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa CAF, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, wabanduliwa
Kombe la Dunia la Wanawake la U-17: Nigeria yaitungua mabingwa watetezi Korea Kaskazini
Marekani mwenyeji wa mashindano ya kwanza ya Wanawake Kombe la Dunia la Klabu FIFA 2028
Liverpool yapindua meza dhidi ya Villarreal kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
CAF yazindua kombe jipya kuelekea Ligi ya Mabingwa ya Wanawake nchini Misri
Zambia na Ghana zapata vipigo katika Kombe la Dunia la Wanawake la U-17
Goli la dakika za mwisho la Madueke lawapa Arsenal ushindi dhidi ya Nottingham Forest
Morocco yaanza kwa ushindi huku Nigeria ikifungwa na Poland katika Kombe la Dunia la Wanawake  U-17
Kombe la Dunia toleo la 10 kwa wanawake U-17 kuanza nchini Morocco
Fifa yaitoza faini Hispania kwa semi za chuki dhidi ya Uislamu wakati wa mechi ya kirafiki na Misri
Infantino aomba radhi kuhusu mpango wa kubinafsisha haki za kibiashara za FIFA
Winga wa zamani wa Barcelona, Chelsea Pedro astaafu soka akiwa na umri wa miaka 39
Ronaldo Ruhsa kurejea kwenye timu kama itampendeza: kocha
Manchester City watapewa adhabu gani?
Rais wa FIFA Infantino aahidi fedha zaidi kwa mashirikisho
Guye na Tigst waongoza Ethiopia kufagia mbio za Berlin Marathon
Mo Salah hatacheza mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Sudan Kusini kutokana na nyasi bandia za Uwanjani