| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Kiongozi wa upinzani Zambia Mundubile ashtakiwa kwa jaribio la mapinduzi
Nyaraka za mashtaka zinasema kuwa Mundubile na mfanyabiashara mmoja walitoa fedha kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi kwa lengo la kupindua serikali.
Kiongozi wa upinzani Zambia Mundubile ashtakiwa kwa jaribio la mapinduzi
PICHA YA MAKTABA: Mundubile na mgombea mwenza walikamatwa muda mfupi baada ya uchaguzi wa urais wa Agosti 13. / Reuters
 

Kiongozi wa upinzani wa Zambia Brian Mundubile na washirika wake wengine kadhaa wameshtakiwa kwa jaribio la kutaka kupindua serikali na sasa Mahakama Kuu itaanza kesi ya uhaini dhidi yao, kulingana na mashtaka waliosomewa mahakamani siku ya Jumatatu.

Mundubile na mgombea mwenza, Makebi Zulu, walikamatwa kwa mahojiano kuhusu madai ya uhaini muda mfupi baada ya uchaguzi wa urais wa Agosti 13, ambao wanadai ulichakachuliwa.

Rais Hakainde Hichilema alishinda muhula mwingine na amekanusha madai ya wizi wa kura.

Mundubile, Zulu na watu wengine 12 wameshtakiwa kwa kupanga njama ya kupindua serikali kati ya Aprili na Agosti 2026, kulingana na nyaraka za mahakama.

Mashtaka hayo yanasema Mundubile na mfanyabiashara mmoja walitoa fedha kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi kwa watu watano kwa lengo la kupindua serikali..

Wakili wa upande wa utetezi, Sakwiba Sikota, anasema mashtaka hayo hayakuwa na msingi na kwamba upande wa mashtaka ulikuwa na “nia mbaya”

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza mapema mwakani, alisema Sikota. Mundubile amewahi kusema kuwa hajahusika na madai hayo na kwamba yamechochewa kisiasa.

CHANZO:TRT Afrika Swahili