| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Maafisa mwanafunzi kutoka nchi 9 za Afrika wahitimu mafunzo ya kijeshi Tanzania
Maafisa hao wamehitimu katika taaluma mbalimbali ikiwemo urubani, udaktari bingwa, uhandisi, ualimu na uchumi.
Maafisa mwanafunzi kutoka nchi 9 za Afrika wahitimu mafunzo ya kijeshi Tanzania
Rais Samia Suluhu Hassan ambae pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu, ameongoza shughuli ya kuwatunuku shahada maafisa hao. Picha/Ikulu Tanzania / TRT Afrika Swahili
 

Maafisa wanafunzi kutoka nchi tisa za Afrika wamehitimu mafunzo ya kijeshi katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) kilichopo Monduli mkoani Arusha nchini Tanzania.

Maafisa hao wamehitimu katika taaluma mbalimbali ikiwemo urubani, udaktari bingwa, uhandisi, ualimu na uchumi.

Wahitimu hao wanatoka Afrika Kusini, Ethiopia, Burundi, Kenya, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Uganda na Zambia.

Rais Samia Suluhu Hassan ambae pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu, ameongoza shughuli ya kuwatunuku shahada maafisa hao.