| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Kenya yaahidi kuyaongezea thamani madini ya Travorite
Mgeni  rasmi wa sherehe hizo alikuwa ni Waziri Mkuu wa Tanzania Mwigulu Nchemba.
Kenya yaahidi kuyaongezea thamani madini ya Travorite
Mgeni  rasmi wa sherehe hizo alikuwa ni Waziri Mkuu wa Tanzania Mwigulu Nchemba. Picha/Hassan Joho / TRT Afrika Swahili
 

Viongozi mbalimbali pamoja na zaidi ya wajumbe 1,700 kutoka duniani kote wamekutana nchini Tanzania katika sherehe ya Usiku wa Madini, ambayo lengo lake ni kufurahia hatua iliyopigwa katika kubadilisha madini na kuyaongezea thamani hadi kufikia bidhaa ya mwisho sokoni.

Mgeni  rasmi wa sherehe hizo alikuwa ni Waziri Mkuu wa Tanzania Mwigulu Nchemba.

Sherehe hiyo pia imehudhuriwa na Waziri wa Madini wa Kenya Hassan Ali Joho ambae ameandika katika ukurasa wake wa X, “Tanzania inajivunia madini ya Tanzanite, madini ya kipekee yanayopatikana Tanzania pekee, Kenya nayo ina Travorite, inayopatika Kaunti ya Taifa Taveta, madini ya kipekee nchini Kenya ambayo tutayaongezea thamani na kuyafanya sehemu ya ukuaji uchumi wetu.”

Mawaziri wengine wa madini waliohudhuria pia ni kutoka Uganda, Rwanda, Ghana, Saudi Arabia na Somalia.