| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Wachimba madini Tanzania watakiwa kutekeleza masharti au leseni zao kufungwa
Ndejembi ametoa onyo hilo alipokuwa akifungua Mkutano wa saba wa Madini na Uwekezaji Tanzania (TMIC), ambao umehudhuriwa na wajumbe 1,715 kutoka zaidi ya nchi 50.
Wachimba madini Tanzania watakiwa kutekeleza masharti au leseni zao kufungwa
Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratius Ndejembi. / Others
 

Serikali ya Tanzania imetishia kufuta leseni za uchimbaji madini kwa wale ambao watashindwa kuendeleza miradi yao

Makamu wa Rais wa nchi hiyo Deogratius Ndejembi amesema serikali haitasita kuzifuta leseni za miradi ambayo imeshindwa kufikia hatua za utekelezaji, wakati ambapo Tanzania inataka kufikia uwezo wake wa sekta ya madini ipasavyo.

Ndejembi ametoa onyo hilo alipokuwa akifungua Mkutano wa saba wa Madini na Uwekezaji Tanzania (TMIC), ambao umehudhuriwa na wajumbe 1,715 kutoka zaidi ya nchi 50.

Amesema miradi mingi ya kimkakati ya uchimbaji, ikiwemo grafili, heli, nikeli na niobium bado haijaanza licha ya umuhimu wake katika uchumi.