Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ametuma salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Naibu Rais wa nchi hiyo Phumzile Mlambo-Ngcuka. Katika ujumbe wake, Rais Ramaphosa amesema, muda mfupi amepokea taarifa za kifo na amehuzunika kwa sababu, alikuwa mzalendo wa kweli aliyeitumikia nchi yake kwa upendo.
Phumzile Mlambo-Ngcuka amewahi kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Makamu wa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 2004 hadi 2008.
Mpaka kifo chake, alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji Umoja wa Mataifa kitengo cha Wanawake chini ya Katibu Mkuu wa UN.
AFRIKA
1 dk kusoma
Rais wa Afrika Kusini amuomboleza Naibu Rais mstaafu Phumzile Mlambo-Ngcuka
Mpaka kifo chake, alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji Umoja wa Mataifa kitengo cha Wanawake chini ya Katibu Mkuu wa UN.

Soma zaidi













