| Swahili
Wafanyabiashara wa DRC wakaribisha kuondolewa kwa ada ya viza kati ya Uganda na DRC
Maamuzi hayo yalikaribishwa na wafanyabiashara nchini DRC, hasa na raia wa mashariki mwa nchi, wenye uhusiano wa karibu sana wa kibiashara na mataifa ya Afrika Mashariki
Wafanyabiashara wa DRC wakaribisha kuondolewa kwa ada ya viza kati ya Uganda na DRC
Uganda / Others
16 Oktoba 2023

Hapo awali, ili kuingia Uganda, Wakongo walilazimika kulipa dola $50 kupata viza ili kukaa kwa miezi mitatu, bila kuhesabu ada ya ukaguzi wa Uviko-19, ambao bado unatumika, ambao ni $45 kuingia Uganda.

Makubaliano hayo kati ya Uganda na DRC, sasa yanaiacha Sudan Kusini, kuwa nchi pekee kati ya nchi saba za Jumuiya ya Afrika mashariki ambayo bado haijawaondoloea raia wa Kongo ada ya viza.

Wakizungumza na TRT Afrika Swahili, wafanyabiashara kadhaa wa Kongo ambao huzuru nchi za Afrika Mashariki, walionyesha kutiwa moyo na hatua hii, ambayo ina uwezo wa kuongeza uchumi kati ya nchi hizo.

"Ni kitu cha kukaribishwa, kwa sababu itatupunguzia gharama. Hatua hii ni kitulizo kwetu, " Amesema Ghislain Muyisa, mfanyabiashara kutoka mji wa Beni mashariki mwa Kongo.

Makubaliano haya yanakuja baada ya Kenya na Tanzania, nchi nyingine mbili za Afrika Mashariki, kuondoa visa kwa raia wa Kongo hivi karibuni.

CHANZO:TRT Afrika