| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Uganda kuulipa Ufalme wa Buganda fidia kwa mali zake zilizotaifishwa
Mali zinazolipiwa fidia ni zile zilizotaifishwa wakati wa serikali ya Milton Obote mwaka 1966 pamoja na Idi Amin.
Uganda kuulipa Ufalme wa Buganda fidia kwa mali zake zilizotaifishwa
Kabaka Ronald Mutebi, mfalme wa Buganda, nchini Uganda—akiwa ziarani wilaya ya Wakiso, mnamo tarehe 18 Septemba 2009. / / Reuters
 

Ufalme wa Buganda nchini Uganda umesema umefurahishwa na hatua ya serikali ya nchi hiyo ya kuanza kulipa fidia ya mali zilizotaifishwa hapo awali na serikali zilizopita.

Waziri wa Habari na Msemaji Mkuu wa Falme hiyo Owek Israel Kazibwe Kitooke amesema hatua hiyo ya serikali, imeiwezesha kuendesha bajeti yake ya kila mwaka, na kufanya uwekezaji katika ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kaunti ya Singo.

Mali zinazolipiwa fidia ni zile zilizotaifishwa wakati wa serikali ya Milton Obote mwaka 1966 pamoja na Idi Amin.

Kufuatia majadiliano ya muda mrefu, na kwa lengo la kuleta usawa katika jamii, serikali iliamua kulipa fidia kwa baadhi ya mali ikiwemo Jengo la Muteesa lililopo London, ambalo lilitaifishwa na kuuzwa na serikali, pamoja na Kiwanja nambari 52 kilichopo barabara ya Kampala, ambacho kilitaifishwa na serikali ya Idi Amin na kupewa Waislamu, ambapo sasa hivi kuna jengo la King Fahad Plaza.

CHANZO:TRT Afrika