Mamlaka ya eneo hilo ya utafutaji na uokoaji imesema katika taarifa yake kuwa moto ulianza kuwaka majira ya alasiri ya Jumamosi katika kiwanda cha "Fonusa Agung Mulia," kilichopo umbali wa takriban kilomita 50 kutoka mji mkuu.
Picha za televisheni zilizorekodiwa usiku zilionyesha moto mkubwa ukiteketeza sehemu ya kiwanda hicho, huku sehemu ya paa ikiporomoka kutokana na moto huo.
Rizki Duyanto, afisa wa mamlaka hiyo ya utafutaji na uokoaji, amesema kuwa shughuli za kuwatafuta watu 39 bado zinaendelea, na kwamba watu wengine wanne walijeruhiwa.
Alieleza kusema kuwa zoezi la uokoaji limekuwa gumu kiasi kwa sababu moto umeendelea kuwaka katika baadhi ya sehemu za kiwanda.
Aliongeza: "Timu zote za utafutaji na uokoaji zinafanya juhudi kubwa kuwatafuta waathiriwa, huku usalama wa watumishi ukipewa kipaumbele."
Kupitia akaunti yake ya Instagram, mamlaka hiyo ilisema kuwa chanzo cha moto huo bado kinachunguzwa.














