| Swahili
ULIMWENGU
1 DK KUSOMA
Israeli yadai kumuua kamanda wa Hamas  Mohammed Deif mjini Gaza
Mashambulizi ya Israeli dhidi ya Gaza yameingia siku ya 300, yakiwa yameua Wapalestina 39,480, wengi wakiwa ni wanawake na watoto na kujeruhi watu 91,128, huku zaidi ya 10,000 wakihofiwa kufukiwa na vifusi.
Israeli yadai kumuua kamanda wa Hamas  Mohammed Deif mjini Gaza
Moshi ukitoka kufuatia shambulio la anga la Israeli katika eneo la Rafah, kusini mwa Gaza, Julai 29, 2024./ Picha: Reuters   / Others

Majeshi ya Israeli yanadai kumuua kiongozi wa kamandi ya Hamas, Mohammed Deif, katika shambulio la anga, mwezi Julai.

Israeli ilimlenga Deif katika shambulio la Julai 13, katika eneo la kusini Gaza katika mji wa Khan Younis, licha ya kutokuwepo kwa uthibitisho wa mauaji hayo.

Zaidi ya Wapalestina 90, wakiwemo wasio na makazi, waliuwawa katika shambulio, mamlaka za afya za Gaza zimesema.

Katika taarifa yake ya Alhamisi, jeshi la Israeli lilisema kuwa “kufuatia tathmini iliyofanyika, tunaweza kuthibitisha kuuwawa kwa Mohammed Deif katika shambulio hilo.”

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika