| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Watalii 183 waliokuwa katika hoteli zilizoungua Zanzibar wapewa hifadhi hoteli nyengine
Hii ni baada ya moto mkubwa kuunguza hoteli sita za kitalii, mighahawa minne na maduka 40 katika eneo la kitalii lililopo wilaya ya Nungwi.
Watalii 183 waliokuwa katika hoteli zilizoungua Zanzibar wapewa hifadhi hoteli nyengine
Waziri wa Utalii Zanzibar Nasra Nassor Omar, amesema watalii 183 wamehamishwa kutoka eneo lililowaka moto na kupelekwa maeneo salama. / TRT Afrika Swahili
 

Waziri wa Utalii Zanzibar Nasra Nassor Omar, amesema watalii 183 wamehamishwa kutoka eneo lililowaka moto na kupelekwa katika hoteli za Mchangani na Matemwe.

Waziri Omar pia amesema, serikali inafanya mawasiliano na balozi mbalimbali ambazo raia wake wamepoteza hati zao za kusafiria kwa ajili ya kupata nyaraka nyengine.

Hii ni baada ya moto mkubwa kuunguza hoteli sita za kitalii, mighahawa minne na maduka 40 katika eneo la kitalii lililopo wilaya ya Nungwi.

Kwa mujibu wa Wizara, uchunguzi wa awali unaonesha moto huo ulitokea jikoni katika Hoteli ya Makofi kabla ya kuenea katika hoteli nyengine jirani, ambazo zilikuwa na mapaa ya makuti.

Ajali hiyo ya moto ilitokea Jumamosi ya Novemba 21. Hakuna vifo wala majeruhi walioripotiwa.

Serikali ya Zanzibar inafikiria kusaidia katika ukarabati wa maeneo yaliyoathirika baada ya tathmini ya usalama kukamilika.