| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
AFCON 2025: Mchakamchaka wa kutafuta nafasi za robo fainali
Mechi za robo fainali zinatarajiwa kufanyika tarehe 9 na 10 Januari, huku fainali zikifanyika Januari 18,
AFCON 2025: Mchakamchaka wa kutafuta nafasi za robo fainali
Nigeria, moja ya timu iliyocheza vizuri hatua za makundi, itakabiliana na Msumbiji. / CAFonline
tokea masaa 16

Hatua ya mtoano ya AFCON inaendelea nchini Morocco siku ya Jumamosi, Januari 3, wakati hatua ya 16 bora ikianza.

Hatua hiyo ya mtoano itaaanza Jumamosi tarehe 3, hadi Jumanne tarehe 6, huku mechi mbili zikichezwa kila siku.

Mechi hizo zinaanza kwa mabingwa wa 2021 Senegal wakikabiliana na Sudan katika uwanja wa Tanger.

Baadaye itakuwa zamu ya mpambano kati ya Mali na Tunisia katika uwanja wa Mohammed V jijini Casablanca, huku Mali wakitafuta ubingwa wao wa kwanza barani Afrika na Tunisia ikitaka kurudia mafanikio yao ya 2004.

Ratiba zingine

Wenyeji Morocco wataingia uwanjani siku ya Jumapili watakapokabiliana na Tanzania uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat.

Wakiungwa mkono na mashabiki wa nyumbani, Morocco itatarajia kubeba taji lake la kwanza la AFCON title katika kipindi cha miaka 50. Wenyeji hao walimaliza wa kwanza kwenye kundi A, lakini Tanzania iliingia hatua hiyo kama mmoja wa timu nne zilizomaliza nafasi ya tatu kutoka kundi C.

Baadaye Jumapili, Afrika Kusini itakabiliana na Cameroon katika uwanja wa Al Medina mjini Rabat. Mpambano utakuwa kocha wa Bafana Bafana Hugo Broos akikabiliana dhidi ya Cameroon, timu ambayo aliiongoza kubeba ndoo ya AFCON 2017.

Jumatatu, mabingwa mara saba Misri watakuwa na Benin katika uwanja wa Agadir. Mara ya mwisho Mafarao kuchukua ubingwa ilikuwa 2010 na watakuwa na hamu kukata kicu chao.

Mechi za mwisho

Jioni ya Jumatatu, Nigeria, moja ya timu iliyocheza vizuri hatua za makundi, itavaana na Msumbiji katika uwanja wa Complexe Sportif de Fès wakijaribu kujiimarisha kutoka nafasi ya pili waliomaliza 2023 kwenye mashindano hayo.

Ratiba ya Jumanne ni Algeria wakivaana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika uwanja wa Prince Héritier Moulay El Hassan mjini Rabat.

Na michuano ya 16 bora itakamilika kwa mabingwa watetezi Côte d’Ivoire kukabiliana na Burkina Faso katika uwanja wa Marrakech.

Robo fainali zimeratibiwa kuchezwa tarehe 9 na 10 Januari, huku fainali ikitarajiwa tarehe 18 Januari katika uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat.

 


CHANZO:TRT Afrika and agencies