| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Hofu yaongezeka miongoni mwa jamii ya Wasomali baada ya Trump kutuma maafisa 2,000 Minnesota
Mamlaka za serikali kuu zinaongeza uwepo wao katika jimbo la Minnesota huku utekelezaji wa sheria za uhamiaji ukiendelea, kufuatia madai yaliyoenea mtandaoni kuhusu udanganyifu katika vituo vya kulea watoto vinavyosimamiwa na Wasomali.
Hofu yaongezeka miongoni mwa jamii ya Wasomali baada ya Trump kutuma maafisa 2,000 Minnesota
Maafisa wa ICE wakiwa katika opareheni za uhamiaji huko Minneapolis, Januari 5, 2026. / / Reuters
6 Januari 2026

Serikali ya Rais Donald Trump imetangaza kutuma takribani maafisa 2,000 wa serikali kuu kwenda Minnesota, hatua inayozidisha kasi ya operesheni dhidi ya uhamiaji katika eneo la Minneapolis–St Paul, kufuatia mvutano mwingine wa kisiasa kuhusu madai ya udanganyifu kwa ustawi wa jamii na huduma za kulea watoto, kwa mujibu wa maafisa.

Kulingana na vyanzo viwili vya vyombo vya sheria vilivyonukuliwa na CNN, maafisa wa Uhamiaji na Forodha (ICE) pamoja na Walinzi wa Mpaka wa Marekani wanapelekwa Minneapolis. Pia, Kamanda wa Uhamiaji wa Marekani, Gregory Bovino, anatarajiwa kuwasili.

Wizara ya Mambo ya Ndani (DHS) imesema ongezeko hilo la maafisa tayari linaendelea.

“Kwa ajili ya usalama wa maafisa wetu hatuelezi kwa kina kuhusu maeneo ya utekelezaji wa sheria, lakini DHS imeongeza nguvu kazi ya vyombo vya sheria na tayari imewakamata watu 1,000 wakiwemo wauaji, wabakaji, wanyanyasaji watoto, na wanachama wa magenge,” alisema Naibu Katibu wa DHS, Tricia McLaughlin, akizungumza na CNN.

Maafisa wa serikali walisema operesheni hii iliyoimarishwa tayari imeanza kutekelezwa.

Mvutano wa hivi karibuni ulizuka mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya video ya YouTuber wa mrengo wa kihafidhina, Nick Shirley, kusambaa kwa kasi, ikidai kuwepo kwa udanganyifu katika vituo vya kulea watoto vinavyosimamiwa na Wasomali. Hata hivyo, maafisa wa jimbo baadaye walikanusha madai hayo, wakisema ukaguzi ulionyesha vituo hivyo vinafanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Tukio hilo limeongeza mvutano wa kisiasa na kufufua matamshi makali ya Rais Donald Trump dhidi ya jamii ya Wasomali wa Minnesota, hali iliyosababisha mashirika ya kutetea haki za kiraia kuonya kuhusu kuongezeka kwa unyanyapaa na hofu.

“Kila mara tunaona mtindo uleule: kuchukua tukio moja, kulihusisha na kundi zima, kisha kutumia hofu kuhalalisha ubaguzi,” alisema Jaylani Hussein, Mkurugenzi Mtendaji wa CAIR–Minnesota.

CHANZO:AA
Soma zaidi
Dunia imepokea vipi shambulio la Marekani nchini Venezuela?
Mashambulizi ya Marekani nchini Venezuela yaliua takriban watu 40: ripoti
Mwanabondia Anthony Joshua arejea Uingereza baada ya ajali ya gari Nigeria
Je, ajenda ya Marekani kubadili mfumo itafanikiwa Venezuela?
Shutuma za kimataifa zaongezeka kutokana na mashambulizi ya Marekani dhidi ya Venezuela
Rais Maduro na mkewe wamelazimika kuondoka Venezuela, anasema Trump
Milipuko yatikisa Caracas kufuatia onyo la Trump la kushambulia Venezuela
Venezuela yawaachia wafungwa 88 wa maandamano ya baada ya uchaguzi
Maelfu waandamana jijini Istanbul kuunga mkono Wapalestina
Israel inataka kufuta vibali vya mashirika ya misaada Gaza na Ukingo wa Magharibi
Watu 6 wameuawa Syria kufuatia shambulio la msikitini wakati wa swala ya Ijumaa
Papa Leo azungumzia madhila ya Gaza katika mahubiri ya Krismasi yake ya kwanza
Papa Leo aadhimisha mkesha wa Krismasi kwa mara ya kwanza kama Baba Mtakatifu
Ubelgiji yajiunga katika kesi ya mauaji ya halaiki ya Afrika Kusini dhidi ya Israel
Marekani yatoa ofa ya $3000 kwa wahamiaji kujiondoa nchini, nyongeza ya mara tatu
Trump awafuta kazi mabalozi 30 wa Marekani katika msukumo wa ajenda ya 'Amerika Kwanza'
Jenerali mwandamizi wa Urusi auawa katika shambulio la gari Moscow
Elon Musk anakuwa bilionea wa kwanza duniani wa $700b baada ya mkataba wa malipo wa Tesla kurejeshwa
Israel yashambulia kwa mabomu harusi ya Gaza na kuua Wapalestina 6 licha ya makubaliano ya amani
Kuzuia mali za Urusi ni 'upuuzi,' Orban aonya wakati viongozi wa EU wakijadili fedha za Ukraine