Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imesema shughuli za uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) zimerudi kama kawaida baada ya ndege iliyotua kwa dharura kuondolewa.
Kwa mujibu wa TAA, ndege aina ya Embraer 125 iliyokuwa ikisafiri kutoka Hifadhi ya Serengeti kuelekea Zanzibar, ilikuwa na abiria 26 na wahudumu wanne.
Ndege hiyo ililazimika kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa KIA, Jumapili asubuhi baada ya kutokea hitilafu katika mfumo wa magurudumu.
TAA imesema hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
.
CHANZO:TRT Afrika Swahili






















