‘Kabla hujafa, hujaumbika’
‘Kabla hujafa, hujaumbika’
Eunice, ambaye kwa sasa ana urefu wa sentimita 59 na uzani wa kilo 26, hakukumbana na changamoto za kimwili wakati wa utoto wake, bali kejeli na kunyanyapaliwa kwa kila namna.
tokea masaa 6

Wakati Josephine Ndunge anajifungua binti yake Eunice miaka 31 iliyopita, hakuwa kwa yake na maneno na mitazamo ya watu baada ya kutoka chumba cha kujifungulia.

“Sikuamini macho yangu, nilishtuka sana baada ya kumuona mtoto wangu,” Josephine anakumbuka.

Kulingana na Josephine, wapo waliomtuhumu kujaribu kutoa mimba, na wengine kudai kuwa alikuwa amelaaniwa asipate mtoto.

Mwanaye alizaliwa bila miguu, hali inayojulikana kitalaamu kama phocomelia.

Eunice, ambaye kwa sasa ana urefu wa sentimita 59 na uzani wa kilo 26, hakukumbana na changamoto za kimwili wakati wa utoto wake, bali kejeli na kunyanyapaliwa kwa kila namna.

“Wako walioniita mtu nusu, niliamini maneno yao…nikajifanya nijichukue,” anaeleza binti huyo mcheshi katika mahojiano maalumu na mwandishi wa makala haya.

Hali hiyo, ilimfanya Eunice awe na mawazo ya kuondoka uhai wake, mara kwa mara.

“Nilijihisi nimefungwa kwenye mwili usio wangu,” anasema.

Tumaini jipya

Hata hivyo, maisha ya Eunice yalichukua mwelekeo mpya wakati mwalimu mmoja alipogundua kuna kitu ndani ya binti huyu, licha ya changamoto ya maumbile yake.

Eunice anakumbuka maneno aliyoambiwa na mwalimu wake, ambaye anamuelezea kama ‘Malaika aliyeshushwa kutoka Mbinguni’.

“Aliniambia kuwa mimi ni wa kipekee sana na ni uwezo wa kufanya yale ambayo hata mtu wa kawaida atashindwa kuyafanya…ilikuwa ni kama kuzaliwa upya,” anasimulia Eunice.

Kwa sasa, dada yake amekuwa msaada wake mkubwa.

"Kuwa dada wa Eunice kimenifundisha maana halisi ya nguvu,” anasema Christine na kuongeza: Kuna furaha kubwa tu kwa kuwa dada yake.

Hata hivyo, Christine ananyong’onyea pindi anapomuona Eunice katika hali ya huzuni, licha ya kuendelea kumpa moyo kila anapopata nafasi.

"Kitu pekee kinachoniumiza ni kumuona akiwa na huzuni. Lakini nimejifunza, hiyo ni sehemu ya maisha. Anaposhindwa kutembea, namwambia, ‘Miguu yangu ni yako.’ Kwa watu wawili, tunayo miguu miwili tu."

Leo hii, Eunice anaishi kwa kujitegemea. Anapika, anafanya mazoezi, na hata anacheza mpira wa miguu, mambo yanayoonesha dhamira yake ya kuishi maisha kikamilifu kwa masharti yake mwenyewe.

Suala la uchumba?

Eunice anakiri kuwa anaye ampendaye.

"Ndiyo, nina mpenzi. Nitakualika nikifunga ndoa,” anasema huku akicheka.

CHANZO:TRT Afrika Swahili