Upinzani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati umeiambia AFP siku ya Jumatano kuwa utasusia uchaguzi wa Disemba ambapo Rais Faustin-Archange Touadera anawania muhula wa tatu.
Viongozi wa jukwaa la upinzani, BRDC, wanasema hawana imani na maandalizi ya uchaguzi huo.
Walikuwa wanapinga uwezekano wa Touadera kugombea muhula mwingine wakati wa kura ya maoni kuhusu katika mpya iliyopitishwa 2023.
Uchaguzi wa Urais, ubunge, serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Disemba 28.
Mazungumzo yaliyokwama
Touadera aliwasilisha rasmi nia yake ya kugombea wiki iliyopita kabla ya siku ya mwisho ya Oktoba 11.
‘‘BRDC haitobadilisha uamuzi wake wa kususia uchaguzi wa Disemba. Hatutoshiriki," mratibu wake Crespin Mboli Goumba amesema, baada ya wito kutolewa wa kufanya mazungumzo na Touadera.
Awali mwaka huu rais alionekana kuwa tayari kwa mazungumzo.
Mkutano wa kwanza ulifanyika mapema mwezi Septemba, lakini hakuna tarehe zingine zilopendekezwa na serikali tangu wakati huo kwa mazungumzo kuendelea.