AFRIKA
1 dk kusoma
Siku ya mapumziko Botswana kusherehekea ushindi wa mbio za Tokyo
Collen Kebinatshipi, ambaye pia alishinda mbio za mita 400, alikimbia vizuri katika mkondo wa mwisho na kujinyakulia medali ya dhahabu wakati Botswana ikiishinda Marekani na Afrika Kusini katika mbio za kusisimua.
Siku ya mapumziko Botswana kusherehekea ushindi wa mbio za Tokyo
Rais wa Botswana ametangaza siku ya mapumziko kusherehekea ushindi katika olimpiki ya Tokyo / AP
tokea masaa 5

Botswana imetangaza siku ya mapumziko kitaifa kusherehekea medali ya dhahabu ya timu yake katika mbio za mita 4x400 kwa wanaume kwenye Mashindano ya Riadha ya Dunia huko Tokyo na kuwa washindi wa kwanza kutoka bara la Afrika kushinda mashindano hayo.

Collen Kebinatshipi, ambaye pia alishinda mbio za mita 400, alikimbia vizuri katika mkondo wa mwisho na kujinyakulia medali ya dhahabu wakati Botswana ikiishinda Marekani na Afrika Kusini katika mbio za kusisimua.

Rais wa Botswana Duma Gideon Boko alitangaza sikukuu kuwa Septemba 29, siku moja kabla ya siku ya uhuru wa nchi hiyo, kuwaenzi Kebinatshipi na wanariadha wenzake Bhekempilo Eppie, Letsile Tebogo na Bayapo Ndori.

"Nitahakikisha kumwambia kila mtu, almasi asilia ya Botswana sio tu ardhini. Ni wanariadha wetu mabingwa wa dunia," Boko alinukuliwa akisema na vyombo vya habari vya ndani siku ya Jumapili.

Baada ya Tebogo kushinda medali ya kwanza ya dhahabu ya Olimpiki ya Botswana katika mbio za mita 200 mjini Paris mwaka jana, nchi yake ilisherehekea ushindi huo kwa mapumziko ya nusu siku.

CHANZO:TRT Afrika and agencies