AFRIKA
2 dk kusoma
Kenya yakamata meli na raia wa Iran wanaoshukiwa kusafirisha dawa za kulevya
Raia sita wa Iran wamekamatwa kwenye pwani ya Kenya mjini Mombasa wakiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya dola milioni 63
Kenya yakamata meli na raia wa Iran wanaoshukiwa kusafirisha dawa za kulevya
Kenya imekamata meli yeney madawa ya kulevya / User Upload
tokea masaa 9

Raia sita wa Iran walikamatwa Jumamosi jioni baada ya Jeshi la Wanamaji la Kenya kukamata meli iliyokuwa ikisafirisha dawa aina ya ‘methamphetamine’, katika pwani ya Kenya, mji wa bandari wa Mombasa ulioko kilomita 485 kusini mashariki mwa mji mkuu Nairobi.

Methamphetamine ni aina ya dawa ya kulevya inayoongeza kasi ya kufanya kazi kwa ubongo na mfumo mkuu wa neva.

Maafisa wa usalama walisema meli hiyo inayoshukiwa kuwa na dawa za kulevya ilisimamishwa wakati wa doria baharini katika Bahari ya Hindi na kusindikizwa hadi maeneo ya ufukweni chini ya ulinzi mkali.

Katika taarifa, Idara ya Upelelezi ya Makosa ya Jinai (DCI) ilithibitisha kwamba maafisa maalum walikamata mamia ya pakiti za mihadarati zilizofichwa ndani ya meli hiyo.

"Mamlaka inachunguza sehemu zilipotoka na zilikuwa zinaelekea wapi methamphetamine hizo za shilingi bilioni 8.2 (dola milioni 63.4)," ilisema taarifa hiyo.

"Uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha vipakiti 769, vinavyotambuliwa kama ‘methamphetamine’," DCI iliongeza.

Maafisa walisema matokeo ya awali yanaonyesha kuwa shehena hiyo inaweza kuwa sehemu ya njia kuu ya usafirishaji wa binadamu inayotumia Bahari ya Hindi kufikia bandari za Afrika Mashariki kabla ya mihadarati kusafirishwa kuendelea.

Washukiwa hao wanazuiliwa mjini Mombasa huku maafisa wa kukabiliana na mihadarati wakiendelea na mahojiano zaidi na uchunguzi wa kitaalamu wa shehena hiyo.

CHANZO:TRT Afrika