Asilimia moja ya eneo la bahari duniani lina miamba ya matumbawe ambapo kuna zaidi ya (asilimia ishirini na tano) 25% ya viumbe vyote vya baharini.
Matumbawe yana umbo la jiwe kama kiunzi cha mfupa wa viumbe waitwao polipu ambayo huchipuka kutokana na kalisiamu kaboneti chokaa inayowekwa na polipu wanapokuwa.
Polipu wanapokufa, mifupa yao hubaki na polipu wengine huota juu ya mifupa mitupu. Baada ya muda mkusanyiko wa mifupa hii hukuwa na kufanya umbo kubwa la jiwe linaloitwa koloni la matumbawe.Kote duniani, mamilioni ya watu wanategemea moja
kwa moja miamba hii kwa chakula na riziki.
Bahari ya Hindi yenye joto karibu na pwani ya Afrika Mashariki ni sehemu ambayo baadhi ya miamba ya matumbawe muhimu zaidi hupatikana.
Hapa visiwa vya Ushelisheli ni mojawapo ya mataifa barani Afrika yenye miamba ya matumbawe. Kwa jumla, kuna visiwa 73 vya matumbawe nchini Ushelisheli.Kisiwa cha matumbawe husababishwa na mabadiliko ya kudumu katika viwango vya bahari.
Kwa vile matumbawe yanaweza kupanda hadi sehemu ya juu ya maji, ikiwa kina cha bahari kitashuka basi kunaweza kupatikana visiwa.
Matumbawe yanasaidia msururu mkubwa wa viumbe vya baharini na yana jukumu muhimu katika kudumisha bayoanuwai ya baharini.
Samaki wengi wanapatikana katika miamba ya matumbawe, pamoja na viumbe vingine vya baharini.Viumbe vya baharini pia hula matumbawe, wakati wengine wakila mwani, inaokuwa kwenye matumbawe.
Viumbe hivi ni pamoja na samaki wa maeneo ya mimea. Samaki wakubwa kama papa huwawinda kwa ajili ya chakula ikiwa ni sehemu ya msururu wa upatikanaji wa chakula kwa viumbe mbalimbali.
Miamba ya matumbawe pia ina jukumu muhimu katika kulinda makazi ya ufukweni kama vile mikoko, ambayo hufyonza kaboni dioksidi kutoka kwenye angahewa yetu na kuihifadhi hadi mara 50 kwa ufanisi zaidi kuliko misitu ya asili.Inafanya kazi kama kizuizi cha asili kwa ukanda wa pwani na mwambao kutokana na mawimbi, dhoruba, na mafuriko hivyo kusaidia katika kulinda maisha na mali za watu.
Ni chanzo kikubwa cha utalii. Matumbawe ni kivutio kwa watalii na wapiga mbizi.Kufikia Septemba 2025 Visiwa vya Ushelisheli vilikuwa vimepokea takriban watalii 300,000 na kuingiza mapato ya zaidi ya(dola milioni mia nane) $800M.
Sehemu kubwa ya mapato haya ni kutokana na shughuli za watu kwenye miamba ya matumbawe kama vile kupiga mbizi.Lakini utajiri huu unatoweka hasa kutokana na
mabadiliko ya tabianchi.
Huko Ushelisheli, janga la El Nino la 1998, pamoja na kimbunga ya Bahari ya Hindi, lilisababisha hasara ya zaidi ya 90% ya matumbawe hai na miamba mingi kuporomoka na baadaye kufunikwa na mwani.
Miongo kadhaa baadaye, tafiti zilionyesha matumbawe hayajarejea kama ilivyokuwa.Hasara zaidi ya 50% ilipatikana baada ya tukio lingine kuu la kuungua kwa matumbawe mnamo 2016.
Mbali na kufifia kwa matumbawe, kuungua kunazuia ukuaji mzuri wa miamba kwa ujumla na uthabiti wake, uzalishaji wa matumbawe na huongeza kuenea kwa magonjwa.
Juhudi za kurejesha utajiri huo muhimu zinaendelea.Kuanzia mwaka wa 2021, serikali ya Ushelisheli
ilunda jopo la usimamizi wa fedha kwa lengo la kulinda miamba.
Lakini juhudi zaidi zinatoka kwa taasisi za sekta binafsi ambazo baadhi zimeanza kutumia mfumo unaoitwa 'ukuzaji wa matumbawe' au'coral gardening', mbinu ambayo inahusisha kukusanya vipande vidogo vya matumbawe vye rotuba, kuvikuza katika vitalu vya chini ya maji na kisha kuvipandikiza kwenye maeneo yaliyoharibiwa.








