Kampuni ya mawasiliano ya Kenya Safaricom ilipata faida kwa asilimia 55 katika faida yake ya nusu mwaka huku ikisema imepata hasara ndogo katika soko lao kuu la upanuzi la Ethiopia.
Safaricom iliorodhesha faida zinazotokana na huduma za shirika hilo kuwa dola milioni 505.62 (shilingi bilioni 65.2 za Kenya) katika muda wa miezi sita hadi mwisho wa mwezi wa Septemba na kuimarisha mkakati wake wa mwaka mzima.
Ukuaji thabiti katika biashara yake ya Kenya uliendelea kuwa kichocheo kikuu cha kuongeza mapato, wakati hasara yake ya nchini Ethiopia ilishuka kwa 59% ikilinganishwa na nusu ya kwanza ya mwaka wa kifedha uliopita, ambayo iliathiriwa pakubwa na kushuka kwa thamani ya sarafu ya birr ya Ethiopia.
Safaricom ilizinduliwa nchini Ethiopia mwaka wa 2022 huku serikali ikifungua uchumi unaodhibitiwa vikali kwa ushindani wa kigeni na inatumai uwepo wake katika nchi ya pili ya Ethiopia, ikitegemea idadi kubwa ya watu barani kuiimarisha ukuaji wa siku zijazo.
Kampuni hiyo ya mawasiliano hisa zake nyingi zinamilikiwa na Vodacom ya Afrika Kusini pamoja na Vodafone ya Uingereza.
Mapato ya huduma yalipanda hadi shilingi bilioni 199.9 katika muda wa miezi sita hadi mwisho wa mwezi wa Septemba, kutoka shilingi bilioni 179.9 katika kipindi kama hicho mwaka uliotangulia, kampuni hiyo ilisema Alhamisi.
Mapato kutokana na huduma ya fedha kwa njia ya simu ya M-Pesa yalipanda hadi shilingi bilioni 88.1 kutoka shilingi bilioni 77.2 hapo awali.













