MICHEZO
1 dk kusoma
Ligi Kuu ya England (EPL) kurindima tena baada ya mapumziko
Ligi Kuu ya England inarejea tena wikiendi hii baada ya mapumziko kwa ajili ya kucheza mechi za kimataifa.
Ligi Kuu ya England (EPL) kurindima tena baada ya mapumziko
Wachezaji wa Arsenal. / Reuters
tokea masaa 18

Mechi za Ligi Kuu ya England zinaanza tena wikiendi hii baada ya wachezaji kumaliza mechi zao za taifa.

Arsenal ambao wanaongoza msimamo wa jedwali sasa hivi wakiwa na alama 16 watashuka dimbani dhidi ya Fulham siku ya Jumamosi. Manchester City watakuwa nyumbani kukabiliana na Everton.

Nottingham watawasubiri Chelsea katika uwanja wao wa City Ground., huku Crystal Palace wakiwa wenyeji wa Bournemouth.

Jumapili waliyo katika nafasi ya pili kwenye jedwali la Ligi Kuu ya England na alama 15 Liverpool watavaana na Manchester United katika uwanja wa Anfield.

CHANZO:TRT Afrika Swahili