Rais wa Kenya William Ruto na rais wa Rwanda Paul Kagame |Photo from State House Kenya 

Kenya na Rwanda zimetia saini mkataba wa makubaliano katika maeneo kumi ya ushirikiano kwa ajili ya kuimarisha mahusiano yao zaidi.

“Ningependa kusisitiza kwamba Kenya na Rwanda zimefurahia uhusiano mkubwa wa urafiki uliojenga msingi imara baina ya watu , kiserikali na hadi kwa biashara,” rais William Ruto alisema katika ziara yake rasmi nchini Rwanda.

Rais Kagame alibainisha kuwa jumuiya ya wafanyabiashara wa Kenya nchini Rwanda imekuwa muhimu katika ukuaji wa uchumi wa Rwanda.

“ ukuaji wa sekta binafsi ni kipaumbele muhimu kwetu. Ushirikiano wa kikanda na biashara ni jambo nyeti kwa ushirikiano huu,” rais Kagame alisema jijini Kigali alipomkaribisha rais Ruto.

Je, Marais wa Kenya na Rwanda waliangazia nini hasa?

  • Ushirikiano katika sekta kumi mkiwemo elimu , teknoloji na maendeloe ya vijana
  • Rais Ruto aliialika Rwanda kutumia bandari ya Mombasa
  • Walikubali kwamba kukosekana kwa utulivu nchini Sudan Kusini, Ethiopia na jamhuri ya demokrasia ya Kongo, DRC kunahitaji kupewa kipaumbele
  • kupanua biashara na uwekezaji pamoja na kusaidia eneo la amani na usalama
  • Kuhusu mzozo mashariki mwa DRC, Rais Ruto alisema kuongezeka kwa wanajeshi kutoka nchi zingine katika kikosi cha Afrika Mashariki ni jambo zuri
  • Rwanda ambayo imekanusha shutuma za DRC kwamba inaunga mkono waasi inasema ni muhimu kuelewa chanzo cha mzozo Mashariki mwa DRC.
  • Rais Kagame amesisitiza jamii ya kimataifa iunge mkono jitihada za viongozi wa kiafrika huku jumuiya ya Afrika mashariki ikijaribu kupata suluhiso kwa mgogoro wa DRC

Rais kenya William Ruto amekua Rwanda kwa ziara ya siku mbili ambapo anatarajiwa kurejea Kenya punde baada ya kukamilisha.

TRT Afrika