9 Desemba 2025
Uturuki imetoa mafunzo ya majini kwa maofisa kadeti kutoka chuo cha mafunzo cha wanamaji wa Libya, ikiwa ni sehemu ya ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili, imesema Wizara ya Ulinzi wa Taifa ya Uturuki siku ya Jumanne.
Kupitia andiko lake lililowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, wizara hiyo ilisema kuwa mafunzo hayo yalifanyika chini ya uratibu wa Kituo Kikuu cha Mafunzo na mji wa Al Khums, ulioko pwani ya Libya.
Mafunzo hayo, ambayo yaliyofanyika kuanzia Disemba 4 hadi 6, yalihusisha mbinu za medani yenye kuongeza kufanisi wa maofisa Kadeti hao.
Washiriki wa mafunzo hayo, walipewa vyeti maalumu wakati wa hitimisho la mafunzo hayo.
CHANZO:AA
















