Ghana imewafukuza Waisraeli 3 siku ya Jumatano, ikiwa ni kisasi baada hapo awali kulalamikia kunyanywaswa kwa kwa raia wake katika uwanja wa Ben Gurion olioko nchini Israel.
“Serikali ya Ghana imewajibika kuchukua hatua hiyo baada ya raia wake kunyanyaswa na Israel…tutaendelea kulinda utu na heshima wetu,” imesema Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.
Kulingana na taarifa ya wizara hiyo, serikali ya Ghana ilimwita Kaimu Balozi wa Israel nchini humo, ili kutafuta suluhu ya mtafaruku huo.
Ghana ilisisitiza kuwa, raia wake wanastahili kupewa heshima kama yale matarajio ya nchi nyingine kwa watu wao waingiapo Ghana.
Mapema Jumatano, serikali ya Ghana ililaani kitendo cha kunyanyaswa kwa raia wake kwenye uwanja wa Ben Gurion nchini Israel, hali iliyopelekea baadhi ya abiria ndani ya uwanja huo kuwekwa rumande.
Kulingana na serikali ya Ghana, raia wake saba, wakiwemo wajumbe kutoka bunge la nchi hiyo, waliwekwa vizuizini bila sababu za msingi, na baada yake kuachiwa, huku wengine watatu wakirudishwa nchini mwao.











