| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Kenya yatoa tahadhari kwa raia wake wanaoishi Uingereza
Kwa wiki kadhaa sasa, Uingereza imeshuhudia maandamano makubwa yaliyoambatana na vurugu na uvunjifu wa amani baada ya wakereketwa wa mrengo wa kulia, kuingia mitaani na kuonyesha chuki dhidi ya wageni na waislamu.
Kenya yatoa tahadhari kwa raia wake wanaoishi Uingereza
Uingereza imeshuhudia maandamano makubwa yaliyoambatana na vurugu dhidi ya wageni na Waislamu. /Picha: Reuters / Others
6 Agosti 2024

Ubalozi wa Kenya nchini Uingereza umewatahadharisha raia wake wanaoishi nchini humo kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo yanayotolewa na serikali ya nchi hiyo.

Kauli hii inafuatia maandamano yanayoendelea nchini humo yaliyoratibiwa na watu wa mrengo wa kulia dhidi ya wahamiaji na waislamu.

“Wakenya wanashauriwa kujisajili katika Ubalozi wa Kenya uliopo nchini Uingereza kupitia tovuti rasmi za Ubalozi,” imesema taarifa ya Ubalozi.

Kwa wiki kadhaa sasa, Uingereza imeshuhudia maandamano makubwa yaliyoambatana na vurugu na uvunjifu wa amani baada ya wakereketwa wa mrengo wa kulia, kuingia mitaani na kuonyesha chuki dhidi ya wageni na waislamu.

Polisi wamekuwa wakijaribu kutuliza hali kwa kushika doria mitaani huku wakisaidiwa na mbwa.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika