| Swahili
AFRIKA
1 DK KUSOMA
'Saa chache' zimesalia mfumo wa afya Gaza kuporomoka kutokana na uhaba wa mafuta
Mashambulizi ya Israeli katika Gaza iliyozingirwa, katika siku yake ya 220, yameuwa takriban watu 35,034 — asilimia 70 kati yao ni watoto wachanga, watoto na wanawake — na zaidi ya 78,755 wakijeruhiwa.
'Saa chache' zimesalia mfumo wa afya Gaza kuporomoka kutokana na uhaba wa mafuta
“There’s nowhere to go. There’s NO safety without a #ceasefire,” UNRWA says. / Photo: AA / AA
13 Mei 2024

Wizara ya Afya ya Palestina katika Gaza imesema mfumo wa afya wa eneo hilo lililozingirwa umebakiwa na 'saa chache' kabla ya kuanguka, baada ya mapigamo kuzuia usafirishaji wa mafuta kupitia vivuko muhimu.

"Tumebakiwa na saa chache kabla ya mfumo wa afya katika Ukanda wa Gaza kuanguka kutokana na uhaba wa mafuta yanayotumika katika kuwasha majenera, gari za wagonjwa na magari ya kusafirishia wahudumu wa afya," imesema wizara katika taarifa yake.

CHANZO:TRT World