Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amepongeza hatua iliyopigwa na Syria baada yam waka mmoja, “licha ya changamoto na hujuma walizokutana nazo.”
Katika chapisho lake lililowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa Uturuki uitwao NSosyal siku ya Jumatatu, Rais Recep Tayyip aliipongeza nchi hiyo kwa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kutokea kwa mapinduzi ya Disemba 8, ambayo alisema kuwa yamewakomboa Wasyria baada ya miaka mingi ya utawala wa kiimla, mateso na changamoto zingine.
Erdogan aliongeza kuwa anatumia maadhimisho hayo kuwakumbuka mashahidi waliouwawa na utawala wa kipindi hicho , akiongeza: “Katika maadhimisho haya, natuma salamu za Uturuki na upendo kwa ndugu zetu Wasyria."
Rais huyo wa Uturuki, pia alisisitiza kuwa nchi yake itaendelea kuipa Syria misaada muhimu, kulinda utawala wake, na kuisaidia kuanzisha amani ya jamii nchini Syria.”
Akiwa ameiongoza Syria kwa kipindi cha takribani miaka 25, Assad alikimbilia Urusi mwezi Disemba mwaka jana, na kumaliza utawala wa chama cha Baath, ambacho kimekuwa madarakani kutoka mwaka 1963.
Hatua hiyo ilianzisha utawala wa mpito, mwezi Januari mwaka huu.















