Burundi deforestation 1

Hifadhi ya Mazingira ya Rukoko nchini Burundi, ambayo ni hazina ya spishi 5,793 za mimea yenye thamani zaidi ambayo ni pamoja na aina 567 zinazopatikana katika eneo hilo, inapigana kile ambacho wanamazingira wanahofia kuwa kinaweza kushindwa dhidi ya upanuzi wa makazi haramu na uharibifu usiodhibitiwa.

Aina ya Hyphaena petersiana (jamii ya mitende) katika Hifadhi ya Kitaifa ya Rusizi, karibu na mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi Bujumbura, inakabiliana na changamoto kubwa ya ukataji miti bila kukoma ili kutoa nafasi kwa makaburi. Sehemu hii ya hifadhi ina urefu wa zaidi ya hekta 10,600 na inaonekana kuathirika zaidi, hasa kwa sababu ya kaya 300 ambazo zimekaa hapo na kusafisha karibu hekta 1,000 ili kukuza mazao.

Katika barabara ya Cibitoke, makaburi ya Mpanda yamepelekea kuondosha kabisa aina hii ya mmea wa kipekee, uitwao "Urukoko" kwa lahaja ya asili. Mtaalamu wa mazingira Emmanuel Niyoyabikoze anakumbuka mkulima Jean Marie Nduwimana akimomboleza kuhusu makaburi yenye sauti ya kifo cha mimea aina ya mitende.

"Hatuna chaguo ila kupanua ufyekaji msitu kwa ajili ya makaburi zaidi," mchimba makaburi wa eneo hilo Jean Marie Nduwimana anaiambia TRT Afrika, akiwa amesimama katikati ya vigogo wa Urukoko vilivyo tapakaa pande zote.

Mnamo mwaka wa 2014, mamlaka ilikuwa imepiga marufuku mifugo mikubwa kutoka Rukoko, hatua ambayo ilionekana kusaidia mimea iliyoachwa kupona kabla ya kuingia makazi ya watu yaliyo athiri sehemu hiyo.

Tishio la kupotea kwa misitu

Tishio la kutoweka spishi hizi za mitende halisababishwi na makazi pekee yanayo ingilia misitu. Useremala, ujenzi na mahitaji ya mkaa ndio vya kulaumiwa kwani vinapelekea misitu minene kupunguzwa na kuwa misitu yenye viraka katika nchi ambayo bado ni miongoni mwa mataifa muhimu zaidi kiikolojia duniani.

Safari ya masoko ya mbao inaonyesha jinsi uharibifu umekuwa mkubwa. Générose Havyarimana, mfanyabiashara, analinganisha mbao zilizotengenezwa kwa miti ya mawese na viumbe vingine vilivyo hatarini.

"Ukiondoa Tanzania, miti hii haipatikani kwa urahisi kwa sasa kwa sababu ya kutoweka kwa aina fulani za miti kutoka kwenye asili yake," anaiambia TRT Afrika.

Kilimo kisichokuwa na kikomo ni kichocheo kingine katika vita vya kumudu maisha ya Rukoko. Ongezeko la uhitaji wa mazao ya chakula kama mahindi na maharagwe, na mazao ya viwandani kama miwa na pamba vimekuwa na madhara kwa aina hii ya spishi, kulingana na Emmanuel. Mashamba ya miwa ya Kampuni ya Tanganyika Business ya Nahum Barankiriza sasa yanachukua sehemu kubwa ya msitu uliokatwa miti hiyo inayo endelea kupungua duniani.

Nini hatma ya mimea hii sasa?

Kutoweka kwa tembo wa mwisho miaka kadhaa iliyopita kunatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu ya kuendelea kupotea kwa Urukoko.

"Kwa kuwalisha matunda ya michikichi, wanyama hawa walishiriki katika kuzaliana kwake ndani ya hifadhi, ambayo bado ina chukuliwa kuwa makazi pekee ya spishi hii iliyo enea," anasema Emmanuel.

Mlo wa tembo ulitokana hasa na tunda la Urukoko, ambalo lina mbegu ambazo hawakuweza kusaga. “Mbegu hizi zilipatikana kwenye kinyesi chake na hivyo kuzaa miti mipya,” anaeleza Emmanuel

Kwa hivyo, wakati "inaongezeka " kwa asili mitende au michikichi ilipata matokeo ya machafuko mbalimbali ya usalama nchini tangu 1993. Ni mwaka wa mapinduzi ya umwagaji damu ambayo yaliiingiza nchi katika machafuko, spishi za mimea pia ziliharibiwa.

Licha ya utofauti mkubwa, mikoa ya milimani inasalia kuwa tete katika suala la uhifadhi endelevu wa rasilimali za misitu ambazo zina thamani kubwa kwa wakazi wa mitaa na mijini.

Kutokana na uharibifu wa Rukoko, Emmanuel anaonya, athari mbaya za kiikolojia ziko karibu kama vile kukosekana kwa utoroshaji wa gesi chafu zinazosababisha mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa ardhi, kuenea kwa jangwa (kukosekana kwa misitu mingine na mapori katika uwanda huu wa Rusizi) na upotezaji wa viumbe hai.

Aina ya miti kama vile Sinarundinaria alpina, Entandrophragma excelsum, Faurea saligna hutafutwa sana, haswa kwa useremala na utengenezaji wa vitu vya sanaa. Baadhi ya spishi hizi zimenyonywa kiasi kwamba kwa sasa zinawakilishwa tu katika sehemu zilizotawanyika za maeneo yaliyo hifadhiwa kama vile Hifadhi ya Kitaifa ya Kibira na Hifadhi ya Msitu wa Bururi.

Wataalamu wa mazingira wanaeleza kuwa katika eneo la Kumoso, spishi nne zinaonekana kuwa vipaumbele vya ukarabati. Hizi ni Pericopsis angolensis, Pterocarpus tinctorius, P. angolensis na Julbernardia globiflora, ambazo zimetoweka kabisa kutokana na unyonyaji mkubwa wa idadi ya watu ambao haujafanya chochote kuwalinda.

Hivi sasa, rasilimali hizi ni chache kiasi kwamba idadi ya watu huenda Tanzania kuzitafuta, jambo ambalo ni tishio.

Jumla ya spishi 40 za mimea kwa sasa ziko hatarini kuto weka.

Shina za kijani

Huku kukiwa na hofu juu ya kasi ya uharibifu wa misitu, kuna mwanga wa matumaini juu ya upeo wa macho. Katika uwanda wa Imbo, spishi zingine huzuiliwa kwenye maeneo yaliyo hifadhiwa. Wanamazingira wanapendekeza uhifadhi wa ex situ katika maeneo matatu ya ikolojia ya nchi ya spishi zinazotafutwa zaidi na wakazi wa eneo hilo, kwa msisitizo maalum juu ya mimea ya milimani.

Bustani tatu za mimea zinazo lenga kutumika kisayansi na uhifadhi zingeundwa, moja katika tambarare ya Imbo, nyingine kwenye ukingo wa Kongo-Nile na ya tatu katika miteremko ya Kumoso ili kukarabati mimea ya kitaifa iliyo katika hatari ya kutoweka kutokana na unyonyaji mbaya.

TRT Afrika