| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Wanafunzi wa kike wa Nigeria waliotekwa nyara watoroka Msituni
Wanafunzi hao walitekwa nyara na watu wenye silaha katika jimbo la kaskazini la Kaduna wiki mbili zilizopita huku eneo hilo likiendelea kukabiliwa na ukosefu wa usalama
Wanafunzi wa kike wa Nigeria waliotekwa nyara watoroka Msituni
Nigeria Students Kidnapped / Photo: AP / AP
19 Aprili 2023

Wanafunzi nane wa kike waliotekwa nyara na watu wenye silaha katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria wametoroka kutoka kwa watekaji wao.

Walikuwa wamezuiliwa na wateka nyara katika ''msitu mnene,'' mamlaka ilisema.

Katika taarifa yake, Kamishna wa Usalama wa Mambo ya Ndani wa Jimbo la Kaduna, Samuel Aruwan alisema mateka hao baada ya kukimbia msituni, wanafunzi hao ''walitembea kwa siku'' hadi eneo.

Kisha ''walihamishwa kwa usalama hadi katika kituo cha kijeshi'' kwa matibabu. Kisha wanafunzi hao wakahamishwa na mamlaka.

Utekaji nyara kwa ajili ya fidia ni jambo la kawaida nchini Nigeria huku magenge yenye silaha yanalenga wasafiri, wanafunzi na jamii za mashambani.

Idadi ya shule, vyuo na vyuo vikuu vimeshambuliwa huku mamia ya wanafunzi wakikamatwa.

Mamlaka imekuwa ikijaribu kukabiliana na ghasia hizo huku wanajeshi wakizidisha mashambulizi ya mabomu katika maficho ya msitu wa magenge hayo.

CHANZO:TRT Afrika