Lionel Messi

Nahodha wa Argentina Lionel Messi amefunga bao lake la 100 la kimataifa kwa mabingwa hao watetezi wa dunia walipoibuka na ushindi wa mabao 7-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Curacao.

Mshindi mara saba wa tuzo ya Ballon d'Or Messi alifunga bao la kuongoza dhidi ya wababe hao wa visiwa vya Caribbean dakika ya 20 huko Santiago del Estero Jumanne.

Hii inakuja miaka 17 tangu alipoifungia timu yake ya Argentina kwa mabao 3-2 dhidi ya Croatia Machi 2006.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, aliongeza jingine baada tu ya nusu saa na kufanya matokeo kuwa 3-0, kisha akakamilisha hat-trick yake dakika ya 37.

Ilikuwa ni hat-trick yake ya saba kwa timu ya taifa.

"Huwezi kumuelezea Messi kwa maneno," alisema mfungaji mwenzake Nicolas Gonzalez.

"Yeye ndiye bora zaidi duniani na anaonyesha mechi baada ya mechi, siku baada ya siku. Kila wakati anapogusa mpira, anakufanya utabasamu."

Messi aliingia kwenye mchezo huo sio tu kama mfungaji bora wa muda wote wa nchi yake, lakini akiwa na mabao mengi zaidi ya wafungaji bora wawili waliofuata -- Gabriel Batistuta mwenye umri wa miaka 56 na Sergio Aguero mwenye mabao 41 – wakiwekwa pamoja.

Hii ilikuwa mechi ya pili ya Argentina tangu kushinda Kombe la Dunia kwa mtindo wa kushangaza dhidi ya Ufaransa huko Qatar mwezi Desemba.

TRT Afrika