| Swahili
UTURUKI
2 DK KUSOMA
Uturuki yanuia kujitegemea katika nyanja ya Ulinzi: Erdogan
"Hatutaacha au kurudi nyuma kutoka katika njia yetu hadi tufikie lengo la Uturuki kujitegemea kikamilifu katika tasnia ya ulinzi," anasema Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Uturuki yanuia kujitegemea katika nyanja ya Ulinzi: Erdogan
Erdogan pia alisema kuwa KAAN, ndege ya kivita ya iliyotengenezwa nchini Uturuki itazinduliwa mwaka 2028, akiongeza kuwa KAAN italinda "anga yetu" siku zote. / Picha: AA   / Others
22 Machi 2024

Uturuki itaendeleza jitihada zake za kujitegemea kikamilifu katika sekta ya ulinzi, rais wa Uturuki amesema.

"Hatutaacha au kurudi nyuma kutoka katika njia yetu hadi tufikie lengo la Uturuki kujitegemea kikamilifu katika tasnia ya ulinzi," alisema Recep Tayyip Erdogan siku ya Ijumaa katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Cankiri nchini Uturuki.

Erdogan pia alisema kuwa KAAN, ndege ya kivita iliyotengenezwa nchini Uturuki, itazinduliwa mwaka 2028, akiongeza kuwa KAAN italinda "anga yetu" siku zote.

Pia alisema kuwa Uturuki imeeanza mipango ya kutengeneza "manowari kubwa zaidi baada ya ile ya TCG Anadolu.”

Erdogan alisema kuwa hakuna mahali salama kwa makundi ya kigaidi, akiongeza zaidi kwamba Ankara hugundua magaidi nje ya mipaka ya nchi, karibu kilomita 300-350 (maili 186-217) na "kuwazuia" "wakati ambao hawatarajii."

CHANZO:TRT Afrika