Mkuu wa Mawasiliano wa Uturuki, Burhanettin Duran, alisema Jumapili kwamba makubaliano ya usitishaji mapigano na ujumuishaji kamili nchini Syria ni hatua muhimu kuelekea kuanzishwa kwa “eneo lisilo na ugaidi,” lengo ambalo limekuwa likisisitizwa kwa muda mrefu na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.
“Utekelezaji wa masharti ya makubaliano hayo utafuatiliwa kwa karibu,” Duran aliandika hayo katika jukwaa la mitandao ya kijamii la Uturuki, NSosyal. Aliongeza kuwa yaliojiri hayakuwa bila mapangilio, bali yanaakisi misingi na onyo ambazo rais amekuwa akizitoa mara kwa mara kwa miaka mingi.
Duran alisema kuwa utulivu wa kudumu nchini Syria unategemea kulindwa kwa haki za matabaka yote kwa misingi ya usawa.
“Syria inayohifadhi uhuru wa mipaka yake na inayojisafisha na mashirika ya kigaidi ni msingi wa amani ya kikanda,” aliongeza, akisema kuwa hatua zinazochukuliwa na juhudi zinazofanywa na serikali ya Syria katika mwelekeo huo ni za muhimu.
Duran alisema kuwa Uturuki ni mshiriki mwenye nguvu mkubwa, iwe ni uwanjani au kwenye meza ya mazungumzo, akibainisha kuwa operesheni dhidi ya makundi ya kigaidi zinasaidia kuunda eneo salama kando ya mipaka ya Uturuki, huku juhudi za kidiplomasia zikiunga mkono michakato inayounda mustakabali wa Syria.
“Uhuru wa mipaka na mamlaka kamili ya Syria ni mambo yasiyoweza kujadiliwa kwa Uturuki,” Duran alisema, akiongeza kuwa Uturuki inaona usalama wa jirani yake kuwa hauwezi kutenganishwa na usalama wake mwenyewe, na inaaamini kuwa amani ni kama kanuni na utulivu linapaswa kuwa lengo.











