| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Jeshi la Sudan linasema limepata mafanikio dhidi ya wapiganaji wanaowaunga mkono RSF
Serikali ya Sudan inasema itaendelea kuimarisha usalama katika miji na maeneo ya kimkakati.
Jeshi la Sudan linasema limepata mafanikio dhidi ya wapiganaji wanaowaunga mkono RSF
Jeshi limetangaza kuharibu vituo kadhaa vya mafuta na silaha. / Reuters
tokea masaa 12

Jeshi la Sudan (SAF) linasema kuwa limewashambulia vikali kundi la wapiganaji wa Al-Dagalo wakati wa operesheni ya kijeshi kote katika eneo hilo kwa siku tatu zilizopita.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu na kusambazwa na shirika la habari la taifa SUNA, jeshi la SAF linasema vikosi vyake vinaendelea kulenga kile wanachoeleza kuwa maeneo ya “magaidi wa wapiganaji wa Al-Dagalo”, likieleza kuwaua kadhaa, kuharibu magari na maeneo yao ya mipango.

Kulingana na jeshi, operesheni sehemu ya Kordofan ilisababisha kuharibiwa kwa magari ya kijeshi 56, pamoja na kuwaua na kuwajeruhi mamia ya wapiganaji.

Katika eneo la Darfur, SAF inasema magari 47 zaidi yaliharibiwa, huku wapiganaji zaidi wakiuawa au wakijeruhiwa katika makabiliano.

Mafanikio mengine ya jeshi

Katika eneo la Blue Nile, jeshi linasema magari manne ya kijeshi yaliharibiwa na kusema waasi kadhaa waliuawa au kujeruhiwa.

SAF pia ilitangaza kuharibu vituo kadhaa vya mafuta na mabohari ya silaha katika maeneo kadhaa, likieleza kuwa mashambulizi hayo yalikuwa pigo kwa shughuli za wapiganaji hao.

Taarifa inasema vikosi vya serikali vinaendelea kuimarisha usalama katika miji na maeneo ya kimkakati, ikiwa ni ishara ya juhudi za kudhibiti maeneo na kuzuia mashambulizi mengine.

“Jeshi bado liko makini kwa lengo la kuwakabili wapiganaji magaidi na kuwaondoa kabisa kote katika nchi,” taarifa ilisema, likisisitiza ari ya jeshi kuendeleza operesheni katika nchi nzima.

Sudan imekuwa katika mapigano tangu Aprili 2023, huku vita kati ya jeshi la Sudan na wapiganaji wa RSF vikisababisha uharibifu, watu kuondoka katika makazi yao, na matatizo makubwa zaidi kwa watu yanayoongezeka.

CHANZO:TRT Afrika Swahili